NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Ndege Tanzania (Air Tanzania) limesema linapitia changamoto za mabadiliko ya ratiba za ndege kutokana na uchache wa ndege zilizobaki uliosababishwa na kuchelewa kwa upatikanaji wa injini mbadala za ndege mbili za Airbus A220-300 kutokana na injini zake kuwa na matatizo.
“Injini mbadala, zinazotakiwa kutolewa na mtengenezaji Pratt & Whitney (P&W), zilitarajiwa kuwasili mwanzoni mwa mwezi Aprili 2023 kutokana na changamoto hizi, tunalazimika kutoa huduma kwa ratiba inayobanana sana ili kukidhi mahitaji makubwa ya wateja wetu.Wakati tunashughulikia changamoto hizi kwa haraka, tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza, kampuni ya ndege itaendelea kuhakikisha inatoa huduma bora ili kufikia matarajio ya wateja wetu;