Ajali yaua wafanyabiashara 13 Songea, haya hapa majina yao

NA DIRAMAKINI

ZAIDI ya wafanyabiashara 13 wamefariki na wengine wawili wamejuruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia Mto Njoka wakati wakitoka Ndongosi mnadani kuelekea Kijiji cha Namatuhi wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Marco Chilya ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 10, 2023 kwenye eneo la chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo Hospitali ya Serikali ya Mkoa Songea (HOMSO).

Amesema kuwa,ajali hiyo imetokea majira ya saa 3, usiku katika eneo la daraja la Mto Njoka Namatuhi katika barabara ya Ndongosi iendayo Namatuhi huko Songea Vijijini.

Amesema kuwa, gari hilo lenye namba za usajili T 800 BXB, Mistubish Fusso, lililokuwa likiendeshwa na dereva Thobias Njovu, lilipofika kwenye eneo la daraja hilo na wakati linapanda mlima ghafla liliacha njia na kutumbukia mtoni.

Amewataja wafanyabiashara walifaofariki kwenye ajali hiyo kuwa ni Happy Msemwa, Jafari Ngalimus, Hidaya Salum,Biesha Yahaya ,Mustafa Ally, wengine wamefahamika kwa jina moja moja ambao ni Mwaisha, Hamad, Juma Said ,Boniface, Christofa Msuya.

Wengine ni Deograsia Mapunda, Simba na mama Faraja ambapo majeruhi ni Hamis Mbawala na Christofa Banda ambao wamelazwa katika Kituo cha Afya cha Mpitimbi.

Kamanda amesema kuwa, maiti zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Songea.

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea kusisitiza wananchi kuacha kupanda magari ya mizigo wanapokuwa wanakwenda kwenye minada hivyo Polisi hawatosita kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayekiuka agizo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news