Askofu akemea ushoga, utoaji mimba nchini

NA DIRAMAKINI

MHASHAMU Askofu Christopher Ndizeye wa Jimbo Katoliki la Kahama mkoani Shinyanga amekemea vitendo vya utoaji mimba na ushoga vinavyoripotiwa kuongezeka miongoni mwa jamii huku akisema huko ni kumkosea Mungu.

Askofu Ndizeye katika mahubiri yake kwenye misa ya mkesha wa Pasaka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga jimboni humo alisema, vitendo vya ushoga na vidhibiti mimba ni vitendo ambavyo ni kinyume cha uumbaji wa Mungu na ni dhambi mbaya.

Pia amesema,ushoga au ndoa za jinsia moja ni kumkosea Mungu na kuzitaka mamalaka husika kuangalia kiini cha tatizo hilo ambalo linaanzia kwenye malezi kwa watoto na uhuru kwa uliopitiliza miongoni mwa jamii.

“Uhai wa binadamu ni kitu kitakatifu na dini na sayansi haziwezi kuwa sawa kwa sababu sayansi ni kugundua, dini yenyewe inafundisha na maadili mema kadri ya mpango wa Mungu na kila sehemu itimize wajibu wake bila kuingiliana,"amesema Askofu Ndizeye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news