Askofu Dkt.Gwajima awasuta wachawi, akemea ushoga na usagaji

NA GODFREY NNKO

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dkt.Josephat Gwajima ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe mkoani Dar es Salaam ameongoza maelfu ya wananchi wilayani Masasi mkoani Mtwara kuvunja nguvu za kichawi, kulaani, kukemea matendo yote maovu ikiwemo ushoga na usagaji.

Mkutano huo mkubwa wa injili ambao umewakutanisha maelfu ya wananchi kutoka pande mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Masasi umefanyika Aprili 3, 2023 huko Masasi mkoani Mtwara.

"Ndiyo maana unaona jini la kutengeneza, linakuwa kama mtu, na ndiyo maana unaona eti siku hizi, mwanaume anaoa mwanaume. Unajiuliza mwanaume ameumbwa wa kutoa, mwanaume ameumbwa ni kama mfano wa Mungu,Mungu anatoa, mwanaume huwa anatoa mbegu, mwanaume huwa hapokei mbegu.

"Mwanaume anaoa kwa sababau anacho cha kuolea, mwanamke anaolewa kwa sababu anacho cha kuolewa. Mwanaume haolewei.Anaolewa wapi...mwanamke anacho cha kuolewa,ndiyo maana wanaolewa. Wanaume wanacho cha kuolea, sasa wanaume wanaolewa,unaolewa wapi, nionyeshe wapi...mambo ya kipumbafu, mambo ya kishetani na hayatakiwi kuwepo katika Taifa letu, na hatutakiwi kuyanyamazia hii ni kuharibu kizazi kijacho, we don't entertain such a foolishness matter. No.

"Hatuyafurahi hata kidogo, sasa mwanamke na mwanamke wanaoana,watazaaje, mwanaume na mwanaume wanaoana, wewe mwanaume unaolewa utazalia wapi, mtoto atatokea wapi, nionyeshe...mbegu zitaingilia wapi na mtoto atatokea wapi, inamaana sasa wanaume kwa wanaume, wanawake na wanawake wakioana hawatazaa, inamaana idadi ya watu duniani itaanza kupungua kwa sababu hatutazaa. Kama wanaume kwa wanaume wanaoana, wanawake wataolewa na nani, kama wanawake kwa wanawake wanaoana tutaona nani,

"Si ubinadamu, tabia za kishetani, Quran Tukufu, kitabu cha Mwenyenzi Mungu haikubali,Biblia Takatifu haikubali.Sheria ya nchi, sheria ya ndoa, Katiba ya nchi inasema ndoa ni kati ya mwanamke na mwanaume. Hatukubali kabisa, yaani hiyo hatukubali kabisa. Na hapa Masasi hatukubali kabisa kwa jina la Yesu.

"Hatukubali kabisa, eh!...mwanaume mwenye ndefu anamuita mwanaume mwingine mwenye ndefu na suti baby!..wee weee weee, si watu,yaani mwanaume hauna aibu, si watu, kwa mauza uza hayo na matatizo hayo wewe ni wewe kweli, muulize mwenzako ni yeye kweli?Hatukubali kabisa,"amefafanua Askofu Dkt.Gwajima.

Katika hatua nyingine, Askofu Gwajima ametoa wito kwa wananchi wote wilayani Masasi na Tanzania kwa ujumla kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku akisisitiza kuishi kwa kupendana bila kubaguana.

"Jamani sisi ni Watanzania, tunajivunia utaifa wetu, tusibaguane, tuishi kwa kupendana,tufanye kazi, msikilize mnayoambiwa na DC wenu wa Masasi,na Mkurugenzi na OCD na viongozi wa Taifa letu bila ukabila, bila udini, tuheshimu viongozi wetu wa Serikali na kufanya kazi kwa bidii. Sawa sawa wana Masasi,"amefafanua Askofu Dkt.Gwajima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news