NA DIRAMAKINI
BABA Mtakatifu Francisco amemteua Askofu Mkuu Protase Rugambwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Congregasio ya Uinjilishaji Vatican kuwa Askofu Mkuu Mrithi (Coadjutor) wa Jimbo Kuu la Tabora.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 13, 2023 na Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 13, 2023 na Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Askofu Mkuu Rugambwa ameshawahi kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma tangu mwaka 2008 hadi 2012 alipohamishiwa Vatican.
"Tunamshukuru Mungu kwa Utume wa Baba Askofu Mkuu Rugambwa,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa leo.
"Tunamshukuru Mungu kwa Utume wa Baba Askofu Mkuu Rugambwa,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa leo.