NA DIRAMAKINI
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema, Sikukuu ya Eid El-Fitri itakuwa kati ya Aprili 21 au 22, 2023 kutegemea mwandamo wa mwezi.
Hayo yamebainishwa Aprili 15, 2023 na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Nuhu Mruma wakati akizungumzia kuhusu mwenendo wa mwezi wa Ramadhani na uwezekano wa siku itakayosheherekea Sikukuu ya Eid nchini.
Sheikh Mruma amesema, sherehe za Eid El-Fitri kitaifa mwaka huu zitafanyika mkoani Dar es Salaam na sala ya Eid itasaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI, BAKWATA makao makuu huko Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Amesema,sala itaanza saa moja na nusu asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika saa 8 mchana katika Ukumbi wa Kimataifa wa The Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuhudhuria.