Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji EAC laanza nchini Uganda

NA MWANDISHI WETU

MKUTANO wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umeanza jijini Kampala.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023.
Meza ya Kuu ya katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023.

Mkutano huo umewakutanisha maafisa waandamizi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki za Burundi, Kenya, Tanzania na Uganda unafanyika tarehe 17 - 18 Aprili 2023. Mkutano huo utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 19 Aprili 2023 na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 20 - 21 Aprili 2023.
Ujumbe wa Jamhuri ya Burundi katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023.

Ujumbe wa Tanzania katika kikao cha Maafisa Waandamizi unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Nazael Madalla. Aidha, ujumbe wa Tanzania unajumuisha ushiriki wa maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania.

Katika kikao hicho, maafisa waandamizi wanajadili na kuandaa nyaraka zitakazojadiliwa katika kikao cha Makatibu Wakuu kinachotarajiwa kufanyika tarehe 19 Aprili 2023 kitakachojadili taarifa nyingine na kupitia utekelezaji wa maamuzi/maagizo ya mikutano iliyopita na Utekelezaji wa Program na Miradi ya Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe maji katika Ziwa Victoria.
Ujumbe wa Jamhuri ya Kenya katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023.

Ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Makatibu Wakuu unatarajiwa kuongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe na kujumuisha ushiriki wa Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Aziz Mlima ambaye atamuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo.
Ujumbe wa Jamhuri ya Uganda katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023.

Tarehe 20 - 21 Aprili 2023 kitafanyika kikao cha Baraza la Mawaziri ambacho pamoja na mambo mengine kitakamilisha Mkutano wa Nne ulioishia ngazi ya Makatibu Wakuu, kupitia, kujadili na kuridhia taarifa ya kikao cha Makatibu Wakuu itakayowasilishwa katika kikao hicho.

Ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Mawaziri unatarajiwa kuongozwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa David Silinde.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news