COSOTA yafafanua hoja ya Mike Tee,waahidi ushirikiano

NA MWANDISHI WETU

OFISI ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Aprili 14,2023 imefanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Tanzania Urban Music Association (TUMA) kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa hoja alizoibua Mwenyekiti wa TUMA, Bw. Mike Tee katika post yake ya Instagram ya Aprili 10, 2023 iliyohoji kuhusu ripoti ya ukaguzi wa hesabu za COSOTA na CAG, Mgao wa Mirabaha na Makusanyo ya Mirabaha yanavyofanyika pamoja na namna Mgao wa Mirabaha unafanyika.
Akizungumza katika kikao hicho Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki, Doreen Anthony Sinare alifafanua kuwa,COSOTA kama Ofisi ya Serikali imekuwa ikikaguliwa na CAG na taarifa ya ukaguzi wa hesabu hizo ni za  wazi na taarifa hizo zinapatikana katika tovuti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

"Kuhusu suala la COSOTA kuendelea kukusanya mirabaha kwa sasa, ni sehemu ya utekelezaji wa sheria kama ilivyoelekeza na jukumu la kukusanya litakabidhiwa kwa Kampuni za kukusanya na kugawa Mirabaha (CMO's) mara baada ya kufanya mgao wa mwezi Juni, 2023 na kuanzia mwezi Julai, 2023 CMO's ambazo zitakuwa zimekidhi vigezo zitaanza kazi ya kukusanya na kugawa Mirabaha hiyo,"alisema Doreen.

Pamoja na hayo Doreen alifafanua pia kuhusu makusanyo ya Mirabaha na Mgao kuwa, COSOTA imekuwa ikitamani kufanya mgao mkubwa ili wabunifu waweze kunufaika na kazi zao. Lakini changamoto ni kwamba wengi wa watumiaji wa kazi hizo wamekuwa hawalipi na pamoja na kwamba operesheni zimekuwa zikifanyika, hivyo aliwasihi wadau hao kuungana na COSOTA katika kipindi cha hivi karibuni kupaza sauti ili kuweza kuhamasisha watumiaji kulipa leseni ya matumizi ya kazi za muziki katika maeneo ya biashara.

Naye Mwenyekiti wa TUMA, Mike Tee na timu nzima waliahidi kutoa ushirikiano katika kuhamasisha makusanyo ya mirabaha kwa kushirikiana na Wanachama wenzao kupaza sauti kwa maeneo ambayo hayalipi yalipe ili mgao ujao uweze kuwanufaisha wadau wengi na wapate viwango vikubwa zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news