Emirate Aluminium Profile yakabidhi tuzo ya Machi kwa Clatous Chama

NA DIRAMAKINI

KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

Katika mwezi Machi, Chama alicheza mechi nne sawa na dakika 273 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa lingine moja.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Chama aliwashukuru wachezaji wenzake, mashabiki na familia kwa mchango mkubwa mpaka kufikia hatua hiyo.

“Nawashukuru mashabiki wachezaji na familia yangu wamekuwa msaada mkubwa mpaka kufanikiwa kupata tuzo hii.

“Hii ni mara ya tatu kwangu kuchukua tuzo hii msimu huu, imekuwa chachu kubwa ikiongozwa na familia yangu, mashabiki na wachezaji wenzangu.

“Kwa niaba ya wachezaji nawashukuru Emirate Aluminium kwa kudhamini tuzo hii anaamini watazidi kuwepo nasi kwakuwa tunawahitaji kwa ajili ya kuongeza hamasa,” amesema Chama.

Chama amekabidhiwa fedha taslimu shilingi milioni mbili na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile kama sehemu ya zawadi ya ushindi huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news