NA LWAGA MWAMBANDE
APRILI 17, 2023 mwanariadha wa Tanzania, Gabriel Gaey aliipeperusha vema bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon 2023 zilizofanyika Boston Massachusetts nchini Marekani.
Mtanzania Gaey katika mbio hizo alitumia saa 2:06:04 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Mkenya Evans Chebet aliyetumia saa 2:05:54.
Mwanariadha huyo wa mbio ndefu wa Tanzania, alidhirisha wazi kuwa, kila penye bidii pana mafanikio, ikizingatiwa kwamba mwaka 2022 katika mbio hizo alishika nafasi ya nne ambapo mwaka huo zilitawaliwa na wanariadha kutoka Kenya kwa upande wa wanaume na wanawake.
Geay mwaka jana alitumia muda wa saa 2:07:53 kumaliza mbio hizo ambazo mshindi alikuwa Evans Chebet wa Kenya aliyetumia saa 2:06:51, akifuatiwa na Lawrence Cherono pia wa Kenya (2:07:21), huku Mkenya mwingine Benson Kipruto akiwa wa tatu kwa kutumia saa 2:07:27.

Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasisitiza kuwa, kwa mafanikio hayo mbeleni kuna nuru na tutarajie makubwa. Endelea;
2:Bendera kapeperusha, Geay twampongeza,
Nchi amewakilisha, Tanzania katangaza,
Pazuri katufikisha, juu tumejisogeza,
Mbele twaona mwangaza, tutazidisha kutisha.
2:Geay jina latosha, jinsi wanalitangaza,
Sisi hiyo yatukosha, upepo livyofukuza,
Matunda kayafikisha, pesa alivyoongeza,
Mbele twaona mwangaza, tutazidisha kutisha.
3:Sabina tano zatosha, Geay twakupongeza,
Hizo utazifikisha, nchi kuiendeleza,
Ukiboresha maisha, peke hutazimaliza,
Mbele twaona mwangaza, tutazidisha kutisha.
4:Pale walitufikisha, kina Bayi papendeza,
Ikangaa wakumbusha, vile walivyoongoza,
Duniani walitisha, na sasa mwatutangaza,
Mbele twaona mwangaza, tutazidisha kutisha.
5:Wote waliowezesha, Geay mbio kuweza,
Sote twapaswa kupasha, hao wote kupongeza,
Ni moto wameuwasha, nchi yetu kutangaza,
Mbele twaona mwangaza, tutazidisha kutisha.
6:Geay moto zidisha kuwasha, na Simbu zidi ongoza,
Medali hazijatosha, nendeni kuziongeza,
Hayo ni yenu maisha, na taifa mwatangaza,
Mbele twaona mwangaza, tutazidisha kutisha.
7:Riadha twawaamsha, juhudi zenu ongeza,
Vijana kuwafundisha, kimataifa kuweza,
Mbali kitufikisha, tutazidi wapongeza,
Mbele twaona mwangaza, tutazidisha kutisha.
8:Timu timu kuanzisha, za riadha tunaweza,
Watoto kuwafundisha, baadaye wataweza,
Nchi kuitangazisha, uchumi wetu kukuza,
Mbele twaona mwangaza, tutazidisha kutisha.
9:Serikai shaonesha, kusaidia yaweza,
Mipango mkifisha, kwa nyie kujiongeza,
Yenyewe mtaikosha, na bajeti kuongeza,
Mbele twaona mwangaza, tutazidisha kutisha.
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602