NA DIRAMAKINI
"Ijulikane kwamba Kabidhi Wasii Mkuu na Msimamizi Mkuu wa Wadhamini anakusudia kwa mujibu wa Sheria ya Miunganisho ya Wadhamini Sura ya 318 toleo la 2002 Kifungu cha 23(1)(d) kufuta Miunganisho ya wadhamini ya taasisi zilizoshindwa kutekeleza maelekezo yaliyozitaka Bodi za Wadhamini za Taasisi kufanya marejeo ya katiba na kuleta marejesho kwa mujibu wa sheria.
"Kusudio hili ni baada ya kipindi cha neema cha miezi sita (6) alichokuwa amekitoa kuisha.
"Kutokana na sababu tajwa, Msimamizi Mkuu wa Wadhamini anautaarifu umma
juu ya kusudio hilo na kwamba katika awamu ya kwanza Bodi za wadhamini 743
zilizoainishwa kwenye tovuti ya Wakala zitafutwa baada ya siku 30 kuisha kuanzia
tarehe ya tangazo hili,"imetolewa Dar es Salaam tarehe 12 Aprili, 2023 na Angela K. Anatory,Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu. Tazama orodha hapa chini;