NA DIRAMAKINI
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesema imebaini ukiukwaji wa Sheria ya Mbolea Na 9 ya Mwaka 2009 uliofanywa na baadhi ya mawakala wanaosambaza na kuuza mbolea hapa nchini.
Aidha, pamoja na uvunjifu huo wa sheria, mawakala hao wamejihusisha na udanganyifu ambao ulikua na lengo la kuisababishia hasara Serikali.
Kutokana na hali hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA,Dkt.Stephan E.Ngailo tarehe 16 Aprili, 2023 ametaja mawakala na vituo vilivyofutiwa usajili wa kusambaza mbolea nchini.
"Hivyo, kutokana na ukiukwaji huo wa sheria tajwa hapo juu, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania unautaarifu umma kuwa, kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa Kifungu cha 14(1)(c) cha Sheria ya Mbolea Na. 9 ya Mwaka 2009 na Kanuni ya 14(1) ya Kanuni za Mbolea za Mwaka 2011, imefuta leseni za mawakala 721 zinazowaruhusu kusambaza na kuuza mbolea nchini kama orodha inavyoonyesha kwenye jedwali;