JE, WAJUA KUMILIKI LAINI YA SIMU ZAIDI YA MOJA NI KOSA NA ADHABU NI KIFUNGO ZAIDI YA MWAKA MMOJA JELA?

NA WAKILI BASHIR YAKUB
+255714047241

HUWA nawaambia kila siku kuwa jambo mpaka likukute ndiyo utajua kuwa lipo. Na nyote si mnajua kuwa kutokujua sheria sio kinga/hoja/udhuru. Hautafikishwa mahakamani ukasema nilikuwa sijui, halipo hilo.

Kanuni ya 18 ya GN. No.112/2020 Kanuni za Mawasiliano ya Posta na simu(usajili wa line za simu) inakataza mtu kumiliki laini ya simu zaidi ya moja kutoka mtandao mmoja.

Kosa hili, adhabu yake ni kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela au faini isiyopungua milioni tano au vyote kwa pamoja. Kwa kipindi hiki tulichomo yawezekana kosa hili ni kati ya makosa yanayotendwa sana na wengi.

Kwa mujibu wa sheria hii, kampuni pekee ndiyo yenye uwezo wa kumiliki line za simu kufikia hadi 30. Mtu binafsi hata line mbili za mtandao mmoja ni kosa.

Hili sio kosa la madai ni jinai tuelewane hapa. Hili jambo ni serious. Wengi mnazo line hadi tano, ni basi tu siku yenu haijafika.

Nyongeza ya adhabu nilizotaja hapa juu, kanuni inasema pia ukikutwa na hatia utatakiwa kulipa shilingi 75,000 kwa kila siku ambayo umemiliki hiyo laini au kila siku ambayo umeitumia.

Kwa hiyo upige hesabu kama umemiliki miaka miwili basi ni shilingi 75,000 mara kila siku katika hiyo miaka miwili. Sikwambiii kama unayo miaka mitano au zaidi.

Hii ni nyongeza ya zile adhabu za juu. Yaani baada ya kupewa zile adhabu za juu sasa unahesabiwa hizo siku ambazo umekaa nayo ili ulipe.Incase mtu anakutafutia kosa hapa hawezi kukukosa. Haya mambo yapo tukipata muda tuelezane tu kama hivi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news