NA DIRAMAKINI
SERIKALI ya Jamhuri ya Kenya imejitolea kutuma kikosi cha maafisa wa polisi nchini Haiti kusaidia nchi hiyo kupambana na ugaidi unaoendeshwa dhidi ya raia na magenge ya waporaji.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Kenya, Mheshimiwa Dkt.Alfred Mutua wakati akijadili hali ya Haiti na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mélanie Joly kwa njia ya simu.
"Tulipitia hali ya Haiti ambapo magenge yamesababisha maisha ya miji na watu kushindwa kuvumilika. Katika suala hili, Kenya imejitolea kutuma maafisa wa polisi kusaidia kuleta utulivu nchini Haiti, ni moja ya mataifa yaliyo mstari wa mbele kuunga mkono mchakato wa Haiti kuelekea utulivu,"Mheshimiwa Mutua alisema kupitia Twitter.
Waziri Dkt.Mutua pia alifichua kuwa mzozo wa Sudan ulijadiliwa siku ya Jumamosi, na kwamba Kenya imejitolea kuwa mpatanishi kati ya makundi mawili yanayopigana nchini Sudan.
"Sote tulitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano na kuheshimu haki za kibinadamu na kuzitaka nchi zinazohujumu amani na utulivu wa Sudan ziache kufanya hivyo mara moja.Aidha, tulikubaliana kusaidiana katika kuwaondoa wananchi wetu,"alifafanua.
Wakati huo huo, Waziri Mutua alisema kuwa ushirikiano wa Kenya na Canada utatoa fursa kwa Wakenya kufanya kazi nchini Canada na pia kufungua fursa za uwekezaji wa pande zote kwa nchi zote mbili.
"Tayari, tunarekebisha mtaala wetu ili kukidhi soko la kazi la Canada, ili wahitimu wa Kenya waweze kufuzu kwa ajili ya kuajiriwa mara moja nchini Canada.
"Tuna nia ya kuvutia wawekezaji wa Canada nchini Kenya na kufungua soko la Canada kwa bidhaa zilizoongezwa thamani kutoka Kenya,"alifafanua Waziri Mutua.