NA LWAGA MWAMBANDE
ZAIDI ya miaka 2000 iliyopita alitokea mwanaume mmoja jina lake aliitwa Yesu, alivyozaliwa na kukua watu wengi walimuona kama seremala kwa sababu baba yake mlezi alikuwa fundi seremala.
Rejea,Mathayo 13:55... "Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?."
Lakini ukweli ni kwamba huyu Yesu alikuwa ndiye mwanakondoo wa Pasaka, Mungu Baba aliupenda ulimwengu akamtoa Yesu aje awe sadaka.
Rejea Yohana 3:16..."Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."
Kwa msingi huo, Mungu alimtoa Yesu, kwa sababu ndani ya Yesu alikuwepo Mungu Neno, kwa kawaida mwanadamu mwingine yoyote asingeweza kufanyika sadaka kwa watu wote, ilibidi apatikane mtu ambaye anauungu ndani yake yaani Yesu.
Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasema kuwa, Yesu ametuhakikishia uzima ndani yetu kupitia damu yake,hivyo ukiomba kupitia damu utapata uzima na kifo cha msalabani kitufikirishe sisi. Endelea;

1.Hili pendo gani kwetu, kufa kwa ajili yetu,
Wenye dhambi sisi watu, abebe mizigo yetu,
Asafishe yote kutu, katika maisha yetu,
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
2.Ni huruma kubwa kwetu, tukiwa katika msitu,
Dhambi kama ukurutu, kutufisha sisi watu,
Bila ya kulipa kitu, kafa kwa ajili yetu,
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
3.Kama siyo Mungu wetu, pendo lake kubwa kwetu,
Kwamba Yesu aje kwetu, huu ukombozi wetu,
Wapi kungekuwa kwetu, tukiwa na wetu utu?
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
4.Mungu amekuja kwetu, kutuponya dhambi zetu,
Ila sisi sisi watu, kwa hii mioyo butu,
Yale mashtaka yetu, limfisha Mungu wetu,
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
5.Huu ukombozi wetu, kutoka kwa Mungu wetu,
Uwe ni sababu kwetu, kuacha mabaya yetu,
Kumfwata Mungu wetu, katika maisha yetu,
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
6.Kuenzi upendo kwetu, kutoka kwa Mungu wetu,
Nasi tuishi kiutu, apendezwe Mungu wetu,
Tusifwate njia zetu, kinyume na Mungu wetu,
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
7.Tungelikuwaje watu, bila kuja Mungu wetu?
Na hii imani yetu, ingefaa nini kwetu?
Tushukuru Mungu wetu, kwa upendo wake kwetu,
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
8.Kufa kwake Bwana wetu, kwenye dunia ya dhambi,
Huko ni kupona kwetu, na tena fahari yetu,
Yesu tumaini letu, kwenye siku zote zetu,
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
9.Kuja kwake Yesu wetu, kumefanya sisi watu,
Tusiokuwa na kitu, sasa tumekuwa watu,
Na katikati ya watu, twapata nafasi yetu,
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
10.Tumpende Mungu wetu, katika maisha yetu,
Kwa hizi nguvu zetu, na hata akili zetu,
Na hii mioyo yetu, iwe kwake Mungu wetu,
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
11.Ni upendo gani kwetu, kutoa uhai kwetu,
Kutuponya dhambi zetu, ziletazo kifo kwetu,
Kwamba hata kufa kwetu, awe ni uzima wetu,
Kifo cha msalabani, kitufikirishe sisi.
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602