NA DIRAMAKINI
OFISI ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema kuna baadhi ya watu wanaotumia ofisi hiyo na jina la Zuhura Yunus kwa barua pepe ya zuhurayunus250@gmail.com kuwatapeli watu na kuwa wanaweza kuwaunganisha kupata teuzi mbalimbali na nafasi za kazi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ikiwataka wananchi kuwaepuka watu hao, kwani ni matapeli.
"Aidha, watu hao kupitia barua pepe hiyo, wamekuwa wakiombwa kutuma kiasi cha fedha ili wapate nafasi za uteuzi katika taasisi mbalimbali serikalini.
"Napenda kuwataarifu kuwa, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu haihusiki na barua pepe hiyo na maamuzi yoyote ya uteuzi. Hivyo, epukeni kutapeliwa mnapopokea ujumbe kutoka kwa watu hao, asanteni,"imefafanua sehemu ya taarifa ya Zuhura Yunus.