NA FATMA JALALA
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeonya uwepo wa vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya Kitanzania kufuatia ongezeko hilo katika vyombo vya usafiri wa Umma nchini ikiwemo mabasi ya Wanafunzi.

"Kumekuwa na matukio ya kuwafanyia vitendo vya kikatili wanafunzi hasa wa kike kwenye mabasi ya Shule, na zipo taarifa za wanafunzi hawa kunajisiwa.Jambo hili halivumiliki na halikubaliki kwa ustaarabu wetu na umma huu wa Watanzania,"amesema Suluo.
Aidha, ameongeza kuwa, kwa sasa wameelekeza, shule zote kuwasilisha orodha ya mabasi yanayotoa huduma kwa shule husika na majina ya madereva, namba za leseni na NIDA.

Suluo amebainisha kuwa, LATRA imekuwa ikitoa matamko kadhaa kukumbusha mazuio ya kikanuni ikiwemo kufanya biashara, mahubiri ya dini na kuweka picha za video na miziki isiyo na maadili ya Kitanzania katika vyombo vya usafiri wa umma.

"Kwa sasa kila mtoa huduma aanze kutathmini video na miziki inayopigwa kwenye magari yake endapo akikaa na mwanae, mzazi wake anaweza kuziangalia au kuzisikiliza? amehoji Suluo.