NA DIRAMAKINI
MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Prof.Elifas Tozo Bisanda amesema Mahafali ya 42 ya OUT yatafanyika Novemba 30, 2023 mjini Songea mkoani Ruvuma.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 25, 2023 na Mhadhiri Mwandamizi, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dkt.Mohamed Omary Maguo.
"Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof.Elifas Tozo Bisanda anayo heshima kubwa kuijulisha jumiya ya OUT na umma kwa ujumla kwamba, Mahafali ya 42 ya OUT yatafanyika Novemba 30, 2023 mkoani Ruvuma mjini Songea.
"Hii ni kufuatia maamuzi ya Baraza la Chuo lililoketi Machi 30, 2023 katika kikao chake cha 115 kuridhia maombi ya Mkoa wa Ruvuma kuwa mwenyeji wa mahafali hayo.
"Hivyo basi, wahitimu wote wanashauriwa kuanza maandalizi mapema ili kufanikisha mahafali hayo. Taarifa zaidi kuhusiana na shughuli hii adhimu tutaendelea kuzitoa kadri muda unavyozidi kusongea. Tunawatakia maandalizi mema na Mwenyenzi Mungu awabariki nyote,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Dkt.Maguo.