NA DIRAMAKINI
MKE wa Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mheshimiwa Angeline Ndayishimiye amewataka wanafunzi nchini humo kuzingatia masomo na kuachana na tabia yoyote ambayo inaweza kuhatarisha maisha yao ya baadaye.
Angeline Ndayishimiye ameyabainisha hayo Aprili 18, 2023 wakati akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya ya Mwaro katika warsha ya uhamasishaji kuhusu afya ya uzazi, ustawi na UVIKO-19.
Katika mafundisho yake, Mke wa Rais aliwaambia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwaro kuwa, kiongozi kijana lazima afikirie maisha yake ya baadaye kwa kufanya maamuzi mazuri leo.
“Lazima uepuke mimba zisizotarajiwa na tabia nyingine yoyote ambayo inaweza kuharibu maisha yako ya baadaye. Epuka kuambukizwa VVU/UKIMWI. Hakuna mustakabali wa maisha bila afya njema,”aliongeza Mke wa Rais.
Katika hotuba yake ya ukaribisho, Gavana wa Jimbo la Mwaro, Kanali Gaspard Gasanzwe alisema kuwa jimbo hilo linafanya kila kitu kuboresha sekta ya elimu.
Pia alionekana kusikitishwa na idadi ya wanafunzi walioacha shule katika jimbo hilo, licha ya jitihada za mamlaka ya utawala kukabiliana na hali hiyo kwa kuwashawishi wanafunzi kupitia maboresho makubwa ya miundombinu shuleni.
Mke wa Rais aliahidi kuendeleza mafundisho hayo kwa vijana kwa nia ya kuandaa Burundi ya kesho yenye wanaume na wanawake wanaostahili na kuwajibika, wenye uwezo wa kusimamia masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini humo.
Katika ziara yake katika Shule ya Sekondari ya Mwaro,Mheshimiwa Angeline Ndayishimiye aliwapatia msaada wa magodoro 150 pamoja na vifaa vingine vya michezo.
Mheshimiwa Angeline Ndayishimiye katika ziara hiyo aliambatana na Waziri wa Afya, Dkt.Sylvie Nzeyimana, mwakilishi mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Burundi na wengine.