MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi ametoa mkono wa Eid El Fitr kwa vituo vya Watoto wenye mahitaji maalum ikiwemo kituo cha Watoto wenye Virusi vya Ukimwi(HIV) Kwarara, Kituo cha Kijiji cha SOS na Kituo cha Watoto Mazizini Unguja katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitr tarehe 22, Aprili 2023.