Mbaroni kwa kukodisha silaha kufanyia uhalifu

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa limemkamata mmoja wa wamiliki halali wa silaha anayetuhumiwa kujipatia fedha kutoka kwa magenge ya uhalifu kwa njia ya kuzikodisha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Allan Bukumbi amesema mtuhumiwa huyo jina lake limehifadhiwa alikamatwa Aprili 3, mwaka huu majira ya saa 11:30 katika eneo la Kihesa Kilimani, mjini Iringa.

ACP Bukumbi amesema, mtuhumiwa ametajwa kukodisha silaha zake hizo aina Shortgun na Rifle pamoja na risasi zake kwa shilingi 100,000 kila moja katika kila tukio la uhalifu jambo ambalo ni kinyume na sheria na utaratibu wa matumizi ya silaha.

“Tunakamilisha upelelezi na wakati wowote kuanzia sasa tutamfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo,”amesema na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi lao kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.

Wakati huo huo, Kamanda Bukumbi amesema jeshi lake linaendelea kumsaka Rashid Nyomolelo anayetuhumiwa kuiba silaha aina ya Pistol Rami pamoja na risasi zake 10 mali ya Joseph Lukonde (44) iliyosalimishwa Aprili 4, mwaka huu karibu na nyumba ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwangata A mjini Iringa.

Pia, Kamanda Bukumbi amesema Polisi wamemtia nguvuni Amani Kasisi (47) mkazi wa Nzihi wilayani Iringa anayetuhumiwa kumlawiti na kumsababishia maumivu makali sehemu za haja kubwa mtoto wake mwenye mwaka mmoja na miezi 10.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news