NA DIRAMAKINI
MBUNGE wa Jimbo la Kaliua Mkoani Tabora Mhe. Aloyce Andrew Kwezi akiwa bungeni Dodoma amesema ardhi ya Vijiji vya Usinga na Ukumbikakoko inapaswa kuendelezwa kama ambavyo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na timu ya Mawaziri 8 walivyoshauri.
Mhe. Kwezi amesema timu ya kufanya tathmini ya kuyagawa maeneo ya Vijiji 2 vya Kata ya Ukumbisiganga ambavyo ni Usinga na Ukumbikakoko. Vijiji hivi vipo tangu mwaka 1974 na Kamati ya Mawaziri 8 walioagizwa na Rais Samia waliwaambia wananchi wasiwe na hofu wakae kwani Rais ameruhusu.
Mhe. Kwezi amesema timu ya kufanya tathmini imekuja na mapendekezo yasiyokuwa na tija kwa Vijiji vya Usinga na Ukumbikakoko kwani agizo la Serikali limesema wananchi wakae maeneo hayo.
Kijiji cha Ukumbikakoko kina Kaya 318 ambazo zimekusudiwa kuhamishwa. Huku kila Kaya itapewa Hekari Tano wakati katika Kijiji chao kila Kaya inakadiriwa kuwa na Hekari 1,000.
Kijiji cha Usinga kina Kaya 937 zilizopendekezwa kuondolewa kwenye kijiji na kupelekwa umbali wa kilomita 42 kutoka zilipo.
Mhe. Kwezi amesema katika Vijiji vya Usinga na Ukumbikakoko kuna miradi ya kimaendeleo inayoendelea kutekelezwa kama mradi wa Maji wa Milioni 440, Zahanati, Shule, Ukarabati wa Reli umeanza kutoka Kaliua kwenda Mpanda na Stesheni ipo maeneo hayo.
Mhe. Kwezi amesema timu ya kufanya tathmini kupitia TFS na TAWA Serikali iipitie upya tathmini ya timu ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi ili miradi ya umeme inayoendelea kutekelezwa isikwame.
Mhe. Kwezi amesema kuna miradi ya Barabara inapita kutoka Mpanda - Kaliua - Ulyankulu - Ushetu - Kahama, wakati kwenye Bajeti kuna pendekezo la kujenga Daraja la Ugala. Maamuzi mazuri yafanyike kusaidia wananchi wa Kaliua.
Mhe. Kwezi amesema Jimbo la Kaliua kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 lina jumla ya wakazi 668,000 ambalo limepakana na hifadhi ya Taifa ya Ugala na Kigosi.