Mchungaji Msigwa aanika marafiki wa aina tano unaopaswa kuwakwepa

Anaandika Rev Peter Simon Msigwa. Endelea;

Kama una rafiki yeyote wa aina moja wapo hapa, achana naye, futa namba yake, block namba yake. Muweke mbali kabisa na maisha yako.

1. Rafiki ambaye kila mara unapokuwa ukisherehekea au kufurahi, hajawahi kuwepo. Lakini kila unapokuwa katika huzuni, au tatizo, hakosekani. 
 
Mtu wa aina hii hufananishwa na mchawi kabisa. Huyu mtu hafurahii unapokutwa na jambo jema lenye heri. Hawa ni marafiki ambao wana wivu na wewe. Hawafurahii kukuona ukishangiliwa au ukipanda. Hawa ni marafiki wa kuwakwepa sana

2. Rafiki ambaye, kila unapotaka kufanya jambo zuri lazima atakukatisha tamaa. Ukisema ‘nataka kuanzisha biashara’ atakuambia, aaah usifanye hivyo bwana. Lazima atakukatisha tamaa unapotaka kufanya kitu kizuri, kitu cha tofauti, kitu ambacho huenda kinaweza kubariki maisha yako. 
 
Lakini rafiki huyu anakupa ushirikiano mkubwa kwenye mambo yasiyo na tija. Kama kwenda klabu, kulewa, na kupoteza muda . Huyu si rafiki sahihi. Anaushawishi ambao sio mzuri. Rafiki wa aina hii mkwepe sana.

3. Rafiki ambaye ni rafiki wa adui zako. Rafiki ambaye ni rafiki wa adui zako ni adui aliyejificha. 
 
Kama rafiki yako yupo karibu sana na watu wanaokuchukia, inamaanisha unaye adui ndani ya himaya yako. Huyu si rafiki mzuri. Ni rafiki ambaye anakuja na sura ya rafiki, lakini nyuma yako ana ajenda ya uovu. 
 
Huyu ni rafiki anayeweza kukusaliti. Kumbuka Yuda alimbusu Yesu mbele ya kadamnasi, lakini alimsaliti kwa siri. Huyu ni rafiki wa kumkwepa sana.

4. Rafiki ambaye kamwe hawezi kukusahihisha. Yaani pale unapokosea, hakwambii kabisa ukweli. Rafiki huyu hawezi hata kukukemea unapokosea. Ajenda yake, ni kukuona ukikosea. Huyu rafiki mkwepe sana.

5. Rafiki wa aina hii, wengi wetu tunaye. Rafiki ambaye huchukua tu na wala hatoi. Huyu rafiki kwa jina lingine anaitwa parasite yeye anachukua chukua chukua tu na wala hatoi. 
 
Atakuja kwako, atakuomba hela, atakuomba nguo atachukua muda wako, lakini yeye hatoi chochote. 
 
Ni rafiki ambaye wewe haufaidiki naye kwa chochote. Kama una rafiki ambaye anachukua tu na wala hatoi chochote, inamaanisha huyu mtu hana mchango wowote katika kufanikiwa kwako. Haupaswi kuwa naye.

Kumbuka, kama una rafiki yeyote kati ya hawa watono, wakwepe sana katika maisha yako.

Ngoja nikupe siri. Kila kitu kibaya kilichowahi kutokea kwenye maisha yako, ukikifuatilia chimbuko lake, utakuta kinahusiana na mtu ambaye umewahi kufahamiana naye kwa namna moja au nyingine. 
 
Simamia sana watu unaojihusisha nao. Watu wabaya wakiondoka kwenye maisha yako, vitu vibaya vitapungua kwenye maisha yako.

Kama maisha yako hayapo kwenye mstari (ugomvi, kesi kila mara, makelele, maneno machafu, n.k) hebu angalia mazingira yako na watu waliokuzunguka.!

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news