NA MWANDISHI WETU
MOJA ya Meli kubwa za kifahari duniani, Seabaorn Sojourn iliyotengenezwa Genoa, Italia, imetua leo Dar es Salaam ikitokea Zanzibar ilikoanzia ziara yake nchini.
Wakiwa hapa nchini, Watalii hao kutoka mataifa mbalimbali duniani baadhi walipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na hapa Dar wametembelea Makumbusho ya Taifa, Kijiji cha Makumbusho, Soko la vinyago la mwenge pamoja na soko la uchoraji Sanaa za Tingatinga.