NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (WAMM), Mhandisi Dkt.Mngereza Mzee Miraji amesema Mpango wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Zanzibar 2022-2027 wenye lengo la kuimarisha sekta ya maji na kumaliza tatizo la maji safi na salama Zanzibar alianzisha kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo mbalimbali.

Alisema katika kipindi ulichoteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini alichukuwa juhudi mbalimbali za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama, kwa kukutana na Mashirika ya Kimataifa ya Misaada ikiwemo JICA, USAID, BPI, Banks ikiwemo AFDB, wawakilishi wa balozi mbalimbali ikiwemo UK, EU, JAPAN n.k.


Mhandishi Dkt Mngereza alisema Miongoni mwa Washirika wa Maendeleo walijitokeza ni pamoja na KFW na GIZ za Ujerumani, Ruden Institute ya Norway, UNESCO-IHI Delft ya Uholanzi, JICA ya Japani na Benki ya EXIM India.
Aidha alimshukuru Rais Mstaafu Jakaya Mrisho, kupitia GWP kwa juhudi zake za kubeba jambo hili kwa hatua zote,alipokuwa Dakar,nchini Senegal aliagiza utekelezaji wa hilo na baada ya muda mfupi alipatikana na kuanza kazi, May-Nov 2022.

Alisema kupitia mashirikiano mazuri na taasisi ya Global Water Partnership, Dkt. Mngereza aliweza kuhudhuria kikao cha dunia cha World Water Forum kule Dakar Senegal ambapo alikutana na wadau wa kimataifa katika sekta ya maji.

Alisema Pia kupitia chuo hicho pamoja na taasisi ya SADC Groundwater Monitoring Institute, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Wizara ya Maji nishati na Madini walianzisha kongamano la kila mwaka la kisayansi kuhusu maji Zanzibar ambalo lilifanyika kwa mara ya kwanza tarehe 14-15 Septemba mwaka 2022 na litakuwa likifanyika kila mwaka.

Vile vile alisema Sera ya maji ya 2004 ina mapungufu kadhaa ambayo inatakiwa kushughulikiwa kwa kufanya mapitio ya hiyo sera. Pia Kunahitajika hatua madhubuti za kuboresha miundo mbinu iliyopo na pia kuongeza miundo mbinu mipya ya kusambaza maji.
Sambamba na hayo hatua madhubuti zinahitajika kujenga mashirikiano na taasisi za kikanda na kimataifa katika sekta ya maji ili kupanua wigo wa mashirikiano ya kitaaluma na utafiti.