NA DIRAMAKINI
MTUME na Nabii Dkt.Peter Nyaga wa Kanisa la RGC Miracle Center lililopo Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam ameandaa sherehe kubwa za kuadhimisha mwaka mmoja wa mafanikio ya Urejesho TV Afrika.
Urejesho TV Afrika inapatikana katika visimbuzi vya Azam TV, Zuku TV, Kwese TV, Nasa Tv, Muvi TV, Signet Kenya, Startimes Kenya na Go TC Kenya.
"Urejesho TV inapatikana kote ndani na nje ya Bara la Afrika, kwa Tanzania katika kisimbuzi cha Azam cha kufanya nenda other chanel,kisha nenda kwenye jina la Urejesho TV na kama hauipati sha kufanya sasa fanya auto search ikishamaliza kufanya auto-seach nenda other chanel, kisha chagua jina la Urejesho TV na ufurahie huduma zetu kwenye ubora wa hali juu,"amefafanua.
Mtume Dkt.Nyaga amefafanua kuwa, sherehe hizo zitafanyika Mei 5, 2023 ndani ya Ukumbi wa Nairobi Cinema uliopo Uchumi House jijini Nairobi nchini Kenya kuanzia saa 12 jioni hadi saa 12 asubuhi.
Mbali na sherehe hizo, pia utafanyika mkesha mkubwa wa kuombea Taifa la Kenya huku maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya Kenya ikiwemo Tanzania wakishiriki.
"Mimi Mtume na Nabii Dkt.Peter Nyaga nitakuwepo Mei 5, 2023 katika mkesha mkubwa wa kuombea Taifa la Kenya ndani ya Ukumbi wa Nairobi Cinema Hall uliopo hapa Nairobi City.Muda ni kuanzia saa 12 jioni hadi saa 12 asubuhi,"ameeleza.
Mwaka jana jijini Dar es Salaam,Mtume Dkt.Nyaga aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, Urejesho TV ni kati ya runinga bora zaidi duniani ambayo itakuwa ikirusha matangazo mubashara kote barani Afrika na duniani kwa ujumla huku lengo likiwa ni kuzidi kuifikia jamii kwa karibu zaidi na kutangaza neno la Mungu.
Alisema, makao makuu ya runinga hiyo yatakuwa nchini Kenya ilipojengwa studio yake ya kwanza na wanatarajia kujenga nyingine hapa Tanzania.
“Kwa televisheni tumeitambulisha na tunataka kufungua studio hapa Dar es Salaam ambapo studio namba moja ipo Nairobi nchini Kenya,namba mbili itakuwa hapa,namba tatu nchini Rwanda,namba nne nchini Burundi tutakwenda hivyo mpaka tufikie nchi saba,“alisema Mtume na Nabii Dkt.Nyaga mwaka jana mbele ya waandishi wa habari.