Nabii Dkt.Mjuni amtamkia baraka zaidi Mheshimiwa Dkt.Ritta Kabati

NA DIRAMAKINI

MTUMISHI wa Mungu wa Huduma ya Yerusalemu Pomerini Ministry iliyopo Kilolo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, Nabii Dkt.Mjuni Kisha amemshukuru na kumtamkia neno la baraka Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa,Dkt. Ritta Enespher Kabati kwa namna ambavyo anaunga mkono injili ili neno la Mungu lizidi kuhubiriwa vijijini na mijini.
Dkt.Mjuni ametoa shukurani hizo baada ya kupokea sadaka ya shilingi milioni moja kutoka kwa Dkt.Kabati ikilenga kuunga mkono injili huko vijijini.

"Ninamshukuru sana Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa,Mheshimiwa Dkt.Ritta Kabati,kwa kunipatia sadaka ya shilingi milioni moja kwenye mkesha wa Pasaka alipomtuma mwakilishi kwa ajili ya kusaidia neno la Mungu liendelee kuhubiriwa kwa kasi huku vijijini.

"Mama huyu anasaidia sana Mkoa wa Iringa, wanajivunia na makanisa mengi hasa ya vijijini ambayo yanajiendesha yanahitaji watu kama mama Rittha Kabati,mimi ninakaa kijijini sana ila milioni moja ilinifuata kijijini,kwa hiyo watumishi tusikimbie kukaa kijijini kuwekeza neno la Mungu,kwani maandiko yanataja kubarikiwa mjini na vijijini. Nami, katika jina la Yesu ninamtamkia neno la baraka Mheshimiwa Dkt.Ritta Kabati, Mungu azidi kubariki kazi ya mikono yake na asipungukiwe kamwe ili aendelee kuwa baraka kwa Watanzania,"amefafanua Nabii Dkt.Mjuni.
Aidha, Nabii Dkt.Mjuni amesema ni jukumu la kila mmoja kushiriki kikamilifu kueneza injili iwe vijijini au mijini ili Mungu azidi kuachilia baraka kwa kizazi baada ya kizazi, kwani "Baraka ya Bwana hutajirisha,wala hachanganyi huzuni nayo."Mithali 10:22.

Nabii Dkt.Mjuni amefafanua kuwa, kuna njia nyingi za kujitoa kwa ajili ya injili. Rejea, Malaki 3:10..."Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la."

Walawi 1:1-2, " BWANA akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng'ombe na katika kondoo."

Hagai 1:8,10 " Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema BWANA. Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake."

Hesabu 30:2, "Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake."

Mtumishi wa Mungu wa Huduma ya Yerusalemu Pomerini Ministry iliyopo Kilolo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, Nabii Dkt.Mjuni Kisha ameendelea kuwa baraka zaidi kwa maelfu ya watu ndani na nje ya Mkoa wa Iringa ambao kila wanapofika kuombea au wanapoombewa na mtumishi huyo wamekuwa wakishuhudia ukuu wa Mungu na wengi wamefunguliwa kwenye vifungo na mateso ya kishetani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news