NA DIRAMAKINI
MTUMISHI wa Mungu wa Huduma ya Yerusalemu Pomerini Ministry iliyopo Kilolo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, Nabii Dkt.Mjuni Kisha amesema, unabii usipowaleta watu kwenye amani,upendo na matengenezo ni kitu katika ombwe.
Pia, manabii wanapaswa kutambua kuwa, wito walionao si kwa ajili ya mtu binafsi kujitukuza bali ni zawadi itokanayo na upendo wa Mungu mwenyewe.
Aidha, kwa kuwa, nabii anatumwa na Mungu basi anapaswa kuwa na uhusiano wa pekee na Mungu. Anapaswa kumsikiliza Mungu ili kwamba ujumbe atakaoupeleka kwa watu usiwe ujumbe wake binafsi bali ujumbe wa Neno la Mungu.
Ndiyo maana kabla ya kumtuma, Mungu alimtakasa Yeremia akamtia wakfu kwa ajili ya kufanya kazi hiyo maalum ya unabii.
"Unabii haupaswi kuwa wa kukisia ila ufunuo wa kweli kutoka kwa Mungu,unabii usipowaleta watu kwenye amani,upendo na matengenezo ni kitu katika ombwe.
"Ushauri kwa watumishi wa Mungu ni vizuri kupitia vipimo kabla ya kuongoza watu kuliko shule peke yake, kwani Musa ilibidi achunge mifugo kabla ya kuchunga watu,na Daudi ilibidi achunge mifugo kabla ya kuongoza watu.
"Mwisho tujitahidi kutofautisha kumwabudu Mungu chini ya Agano la Kale na kuabudu katika Agano Jipya,na chombo cha mwisho kulinda watu wake ni Serikali,tuendelee kuwa wazalendo kwa nchi yetu kuibua hata vitendo viovu kucheza na akili za watu,"amefafanua Nabii Dkt.Mjuni.