NA BEATRICE MAINA
NABII Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie ambaye pia ni Balozi wa Amani ametoa wito kwa waandishi wa habari hapa nchini kuhabarisha habari zenye tija katika jamii na kuacha kuchapisha picha na kutoa habari zinazodhalilisha viongozi wa nchi.
Ametoa wito huo alipokuwa akifundisha katika ibada ya Chuo Kikuu cha Manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko Ngurumo ya Upako Kisongo jijini Arusha.
Dkt.GeorDavie amesema kuwa, kuna vitu vya kustahi kwa Kiongozi maana ni alama yako na kuongeza kuwa lazima kusitiri viongozi wa nchi.
"Waandishi wa habari acheni kupelekea habari mbaya za viongozi wenu,"amesema Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie.
"Waandishi wa habari acheni kupelekea habari mbaya za viongozi wenu,"amesema Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie.