Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Segerea yajiridhisha na upatikanaji maji jimboni

NA DIRAMAKINI

LEO Aprili 13, 2023 uongozi wa Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Segerea mkoani Dar es Salaam umetembelea ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa Tabata kwa malengo ya kujua maendeleo ya huduma ya maji ya DAWASA jimboni Segerea.
Akiongea na Katibu wa Mbunge, Mhandisi wa Maji Mkoa wa Tabata, Agnes Mtelekesya ameeleza kuwa,DAWASA Tabata inahudumia kata tisa jimboni Segerea ambazo ni Segerea, Liwiti, Bonyokwa, Kisukuru, Kimanga, Tabata, Mnyamani, Vingunguti na Kipawa.

Mhandisi Agnes ameeleza kuwa upatikanaji wa maji katika kata saba za Kipawa, Vingunguti, Mnyamani, Tabata, Kimanga, Liwiti na Segerea ni wa asilimia 100 na maji yanapatika katika kata hizo saa 24 na siku zote saba za wiki.

Aliendelea kueleza kuwa, kata za Kisukuru na Bonyokwa huduma bado haijakaa sawa na kwa sasa wanapata maji kwa mgao wa siku moja kwa Juma.

Mhandisi Agnes aliendelea kueleza kuwa,katika kata hizo upo mradi mpya utakaojulikana kwa jina la MRADI WA BANEBANE ambao utalazwa bomba za nchi nane na utapita maeneo ya Banebane, Luhanga, Jumba la dhahabu, Katoma na Mkuwa.

Utekelezaji wa mradi huo utaanza mapema Jumatatu ya April 17, 2023.Kukamirika kwa mradi huo kutasaidia kuongezeka kwa maji katika kata hizo na hivyo mgao wa maji kupungua na ikiwezekana kuisha kabisa.

Katibu wa Mbunge,Mwalimu Lutta Rucharaba amemshukuru Mhandisi huyo na kuahidi kushiriki katika ulazaji wa bomba wiki ijalo.

Kata zilizobaki nne yaani Kinyerezi inahudumiwa na DAWASA KINYEREZI, Buguruni inahudumiwa na DAWASA ILALA na Kiwalani na Minazi Mirefu zinahudumiwa na DAWASA TEMEKE na zitatolewa taarifa baadaye.

Kufuatia taarifa hii ya huduma ya maji jimboni Segerea kuimarika, Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mhe. Bonnah Ladislaus Kamoli amemtumia salaam za pongezi na shukrani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo anayoendelea kuifanya, lakini pia Waziri wa Maji,Mhe.Jumaa Awesso kwa usimamizi uliotikuka.

Hata hivyo, ziara ya Katibu wa Mbunge inaendelea na kwa sasa anaelekea mtaa wa Tenge Kata ya Tabata.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news