Ongezeni nguvu kusimamia elimu-Dkt.Msonde

NA FRED KIBANO

SERIKALI imewaagiza maafisa elimu wa mikoa na halmashauri nchini kuongeza nguvu ya kusimamia elimu, umahiri, ujuzi na maarifa wanayoyapata watoto ili kuendelea na masomo yao pasipo vizuizi.
Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Charles Msonde ameyasema hayo hivi karibuni wakati wa kufunga wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara (REDEOA) jijini Mwanza.

“Katika changamoto ambazo zinawakabili watoto wetu kule shuleni ni ubakaji, ulawiti, usagaji na vitu vingine, sisi walimu na sisi Viongozi wa walimu na walimu wote nchini dhamana ya kuliweka na kulitengemeza Taifa na kuwasimamisha watoto hawa wawe na maadili, uzalendo na utu wema tumewa hilo jukumu sisi.”

Dkt.Msonde amesema , pamoja na kuwepo kwa mafanikio ya ufuatiliaji wa elimu nchini bado zipo changamoto kadhaa ambazo Viongozi hao wanapaswa kushughulika nazo kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na kufuatilia ufundishaji sio tu eneo la Shule na Ufundishaji lakini pia namna mtoto anavyopata umahiri na kumudu masomo yake lakini pia wao wenyewe kuacha kufuatilia kwa mazoea kwani wamepewa dhamana ya kuhakikisha Elimu Bora inatokea katika Taifa la Watanzania.

“Bado ipo changamoto ya ufuatiliji dhaifu miongoni mwetu sisi, watanzania wametupa dhamana kufanya kazi hii ya kufanya ufuatiliaji makini ya kuhakikisha walimu wetu wanafundisha na umahiri wa watoto wetu unapatikani.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Vicent Kayombo amesema katika mkutano wao Viongozi hao wamekubaliana kuwa baada ya kikao kazi hicho watakwenda kuongea na walimu shuleni, wanatarajia kwenda kufanya mapinduzi ya Ufuatiliajiwa wa ufundishaji wa walimu darasani lakini pia kuendeleza ushirikiano wa kisekta kati ya Maafisa Elimu Msingi na Sekondari, Wathibiti Ubora, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) na wengineo ili kuwa na uelewa wa pamoja na kufanya kazi kama timu.

Kikao kazi hicho cha mwaka cha siku tatu kiliambatana na utoaji Tuzo za Viongozi waliofanya vizuri na Wadau waliofanikisha mkutano huo pia lengo lake ni kufanya tathmini ya kina na kuja na mbinu mbadala katika kutatua changamoto za elimu nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news