OR-TAMISEMI YAWAPONGEZA WANANCHI WA SUJI UJENZI WA NYUMBA YA MTUMISHI WA ZAHANATI

NA OR-TAMISEMI

TIMU ya Usimamizi Shirikishi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) imewapongeza wananchi wa Kata ya Suji, Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro kwa kujenga nyumba ya mtumishi na kushiriki katika ujenzi wa Zahanati ya Suji Malindi.
Pongezi hizo zimetolewa Aprili 25, 2023 na Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Dkt. Ntuli Kapologwe kwa niaba ya timu hiyo baada ya kutembelea na kukagua utoaji wa huduma za afya katika zahanati hiyo.

"Tuwapongeze sana kwa kujitoa katika utekelezaji huu, tumeziona jitihada zinazofanywa na wananchi wa Kata hii katika kuunga mkono azma ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ,changamoto zilizobainishwa tumezichukua na kuona namna bora ya kuzitafutia ufumbuzi kama Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI," amebainisha Dkt.Kapologwe.
Pamoja na pongezi hizo, Dkt.Kapologwe amewataka watoa huduma wa zahanati hiyo kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi wa Kata ya Suji huku akisisitiza kuwa uimarishaji wa miundombinu uendane na utolewaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

Naye, Diwani wa Kata ya Suji Malindi Mhe. Edith Banzi amebainisha kuwa pamoja na kuchangia nguvu kazi hizo wananchi hao wameandaa tofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba nyingine ya watumishi watakaotoa huduma katika zahanati hiyo.
Kwa upande wake, Wilfred Kiboko amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kuboresha huduma za afya msingi nchini amemhakikishia kuwa wananchi wa Kata ya Suji wapo tayari kuunga mkono juhudi hizo ili kila mwananchi anufaike na mafanikio yanayopatikana.

Timu hiyo ya usimamizi pia ilitembembelea Hospitali ya Wilaya Same,Kituo Cha Afya Vunta, Kituo Cha Afya Shengena pamoja na Zahanati ya Suji Gonjanza

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news