Polisi, TAWA wanasa meno 28 na vipande 62 vya tembo

NA DIRAMAKINI

KAMANDA wa Jeshi la Polisi mkoani Lindi, ACP Pili Mande amesema,jeshi hilo kwa kushirikiana na wahifadhi wanyamapori wa M
amlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA) wamekamata watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo mazima 28 vikiwemo vipande 62.

Ameyasema hayo ofisini kwake mjini Lindi wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akiwataja waliokamata kuwa ni Said Seleman Litangulu (55), Selemani Hassan (32) na Bakari Said (22) wakazi wa Kijiji cha Nanjilinji kilichopo wilayani Kilwa mkoani hapa.

Wakati huo huo ACP Mande amesema,Jeshi la Polisi mkoani hapa limewakamata watu 122 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na nyara za serikali kama vile nyama ya nyati, dawa za kulevya aina bangi,pombe haramu ya gongo, wizi wa mali zikiwemo runinga, simu na pikipiki

Naye Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi kutoka M
amlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA),Kennedy Sanga amesema, meno na vipande hivyo vinaonesha ni takribani tembo 30 waliuawa.

Sanga amesema, hali hiyo inaharibu mfumo wa uhifadhi huku akiwataka wakazi wa maeneo hayo kuacha mara moja matukio hayo, kwani ni makosa ya kiuhujumi uchumi ambapo tayari wameshaandaa mipango kuwadhibiti wanaohusika na ujangili huo ndani na nje ya mkoa huo.

Kwa nyakati tofauti wananchi mkoani Lindi wameieleza DIRAMAKINI kuwa, jitihada za pamoja katika kulinda na kukabiliana na wahalifu wanaohatarisha hifadhi na wanyamapori nchini zinapaswa kuungwa mkono na kila mmoja ili kuhakikisha maliasili za Taifa zinaendelea kudumu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news