Prof.Nagu aitaka Hospitali ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi ya Kibongóto kuwasilisha mpango kazi wa matokeo ya utafiti

NA MWANDISHI WAF 

MGANGA Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ameitaka Hospitali ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi ya Kibongóto kwa kushirikiana na Mtandao wa Watu Waliougua Kifua Kikuu na Kupona (MTUKTA) kuhakikisha wanakuja na mpango kazi wa kufanyia kazi matokeo ya utafiti wa mwaka mmoja uliofanyika wa kuchunguza watu waliowahi kuugua kifua kikuu na kupona lakini baada ya kupona hawakufatiliwa kwa karibu.
Prof. Nagu ametoa wito huo leo jijini Dodoma katika ufunguzi wa kikao kazi cha usambazaji wa matokeo ya mwaka mmoja ambao umeweza kushirikisha watu waliowahi kuumwa kifua kikuu na kupona lakini baada ya kupona wakawa hawafuatiliwi kwa karibu kujua maendeleo yao.

Prof. Nagu amesema kuwa wanatakiwa kuwasilisha mpango kazi kwa wizara kulingana na matokeo waliopata kutoka katika utafiti huo uliofanyika ili kuhakikisha wanaongeza umakini dhidi ya maambukizi ya kifuu kikuu nchini.

Naye, Mkurungenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi ya Kibongóto iliyopo Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Leonard Subi amesema kuwa kupitia utafiti huo wameweza kupata zaidi ya watu 625 ambao walikuwa katika jamii na watu hao wamefanyiwa uchunguzi tena kuona kama hawana kifua kikuu.
“Katika watu 625 tulio wafanyia uchunguzi tumeweza kugundua asilimia 24 kati yao tayari walishaugua tena kifua kikuu na wapo katika jamii na watu 8 walikuwa ni wale walio na kifua kikuu sugu,"amesema Dkt. Subi.

Hivyo ametoa rai kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kushirikisha jamii hususani katika kuwafuatilia kwa ukaribu watu waliougua kifua kikuu na kupona ili kujua maendeleo yao katika jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news