NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Dkt.Rukia Rajab Bakari kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 4, 2023 na Kaimu Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Dkt.Juma Yakuti Juma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Dkt.Rukia ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Kampasi ya Sayansi za Afya Mbweni katika Idara ya Uuguzi na Ukunga umeanza leo Aprili 4, 2023.