NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewatakia heri na baraka za Sikukuu ya Eid El Fitr waumini wa dini ya Kiislamu na wananchi wote kwa ujumla.
Baadhi ya wananchi wakiwemo watu wenye ulemavu, wazee wasiojiweza, yatima, wajane na walimu wa madrasa wakifurahia sadaka ya Eid El Fitr kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi alizowagawia leo Aprili 21, 2023 katika Msikiti wa Jamiu Zinjibari Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi. (Picha na Ikulu).
Salamu hizo amezitoa kupitia taarifa iliyotolewa leo Aprili 21, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hillary.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi anaamini sikukuu hii itakuwa ni fursa kwa Waislamu wote kuw apamoja kusherehekea Sikukuu ya Eid kwa amani.
Sambamba na kuwasaidia wengine ambao hawana uwezo na wenye mahitaji maalu, kwani kufanya hivyo ni miongoni mwa nguzo muhimu za dini ya Kiislamu.
Hata hivyo,Eid El Fitr ni sherehe yenye furaha inayoadhimishwa na Waislamu kote duniani kumalizia mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.