NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaji Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameendelea kutoa sadaka kwa watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye ulemavu,wazee,yatima na wajane katika maeneo mbalimbali kisiwani Unguja na Pemba.
Pia, Mheshimiwa Rais Alhaji Dkt.Mwinyi ameendelea kuzishukuru taasisi za Serikali na watu binafsi kwa michango yao na kwa sadaka walizochangia kufanikisha kuwasaidia sadaka watu wasiojiweza katika jamii nchini.
Aidha, Mheshimiwa Rais akiwa na mke wake,Mama Mariam Mwinyi kwa nyakati tofauti wameshiriki katika futari maalumu alizowaandalia yatima, walimu wa madrasa,masheikh,wajane,walemavu na wazee Pemba na Unguja.
Kupitia, hafla hizo, Rais Dkt.Mwinyi amekuwa akiwahimiza waumini wa dini ya Kiislamu kuongeza jitihada kwa kufanya ibada, kuendelea kudumisha umoja, upendo na mshikamano kwa ustawi bora wa familia, jamii na Taifa.
Zifuatazo chini ni picha mbalimbali zikionesha Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi, Mama Mariam Mwinyi wakishiriki kutoa sadaka na futari maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba;