Rais Dkt.Mwinyi:Serikali inafanya juhudi kuimarisha miundombinu na mazingira ya huduma za usafiri wa baharini

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema usafiri wa baharini ni muhimu katika nchi kama Zanzibar, na Serikali inafanya juhudi za kuimarisha miundombinu na mazingira ya huduma za usafiri wa baharini. 
Pia, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinnyi amewashukuru wawekezaji wa Azam Marine kwa kuleta vyombo vya usafiri wa baharini vyenye ubora, na kueleza kuwa mchango wao ni muhimu katika kurahisisha huduma za usafiri wa baharini. 
Ameongeza kuwa, ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma una umuhimu katika kukuza uchumi na kuimarisha huduma za jamii ikiwa ndio malengo ya Serikali.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Aprili 24, 2025 wakati wa uzunduzi wa boti mpya Kilimanjaro VIII ilizinduliwa rasmi katika Hoteli ya Verde, Mtoni jijini Zanzibar.
 
Rais Dkt.Mwinyi amesema, malengo ya Serikali ni kuzipatia ufumbuzi wa muda mrefu changamoto zitokanazo na msongamano wa abiria , ufinyu wa nafasi wa bandari kuu ya Malindi kwa kutekeleza mradi wa ujenzi kisasa wa Ferry Terminal eneo la Maruhubi kwa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi. 
 
Pia, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameiomba Kampuni ya Azam Marine kufanya safari kati ya Unguja na Pemba ikiwezekana na Tanga katika kuwarahisishia wananchi huduma za usafiri. 
 
“Ombi langu kwenu ni kwamba, tuna uhaba mkubwa wa usafiri wa Unguja na Pemba, ninaomba kwa sababu mumeongeza vyombo basi kuwe na safari maalumu za Unguja na Pemba, wananchi wa Pemba wangependa kutumia muda mfupi, vyombo wanavyotumia sasa vinachukua muda mrefu sana na pia havipo siku zote, tunaomba Azam mtusaidie kupunguza hili tatizo wakati Serikali inajipanga kufanya kwa upande wake.”

Amesema, safari za Unguja, Pemba na Tanga ni muhimu kwa kutoa huduma kwa wanachi. Pia, Rais Dkt. Mwinyi alieleza Serikali inathamini mchango wa sekta binafsi katika utekelezaji wa mipango ya serikali ya maendeleo na ukuzaji wa uchumi.

Alitumia fursa hiyo kuzihakikishia kampunzi za Bakhresa kupata ushirikiano kutoka serikalini ili miradi waliyowekeza kuona inaleta faida kwao na nchi kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Rais Dkt.Mwinyi aliziagiza, Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA) washirikiane na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini ya Tanzania Bara (SUMATRA), kuongeza ufanisi na kuhakikisha usalama wa vyombo vya usafiri wa baharini unaendelea kuwepo.

Pia amesema, Serikali kwa awamu zote za uongozi, imejitahidi kuimairisha miundombinu na mazingira mazuri kwa kutoa huduma bora za usafiri wa baharini pamoja na wajibu wa kusimamia usalama wa abiria na mizigo kwa vyombo vinavyotumia usafiri huo.

Dk. Mwinyi, aliwanasihi wananchi kuacha kutumia vyombo vya usafiri wa baharini visivyozingatia usalama wao na kuacha kutumia bandari bubu kwani kunahatarisha maisha yao na ni kinyume cha sheria.

Akizingumzia ufinyu wa bandari ya Malindi, Rais Dk. Mwinyi alieleza Serikali imechukua jitihada kuimarisha eneo kupunguza msongomano wa abiria kwa kuipatia ufumbuzi wa kudumu changamoto hiyo kwa kutekeleza mradi wa Ferry Terminal katika eneo la Maruhubi kwa kujenga kituo kipya cha kisasa kwa ushirikiano wa Serikali na Sekta binafsi.

Aidha, Dkt.Mwinyi alieleza bandari ya Malindi baada ya shughuli za mizigo kuhamia bandari ya Mangapwani itatengenezwa upya ili iendane na dhamira ya Serikali ya kuufanya Mji Mkongwe na maaneo yake kuwa sehemu maalum ya kuendeleza Sekta ya Utalii.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Uwekezaji, Mudrik Soraga alisema Serikali imejipatia mafanikio makubwa kwenye sekta ya uwekezaji na kufanikiwa kuleta wawekezaji wenye mitaji mikubwa ya zaidi ya dola za Marekani 373.5 na tayari imesajiliwa.   

Naye Mkurugenzi wa Azam Marine, Abubakar Azizi amesema kampuni zao zimewekeza mtaji mkubwa wa zaidi ya dola za Marekano milioni 120 ili kuwafikishia huduma bora Watanzania pamoja na wageni wanaotembelea nchini kupitia sekta zake za biashara.

Amesema, boti ya Kilimanjaro VIII “The Falcon of Sea” ina uwezo wa kuchukua abiria hadi 11, 000 kwa siku, ina madaraja ya VIP, Royal na daraja la kawaida.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news