Rais Dkt.Ruto awashukuru washirika wa maendeleo

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Kenya, Dkt.William Ruto amewapongeza washirika wa maendeleo kwa mchango wao katika afya ya umma nchini Kenya.
Amesema ushirikiano wa karibu na wenye nguvu umewezesha Kenya kushinda magonjwa kama vile Malaria, VVU/UKIMWI na Kifua Kikuu.

Mheshimiwa Rais Dkt.Ruto alielezea Mfuko wa Kimataifa kwa ushirikiano wake ambao umeendeleza utambuzi wa Bima ya Afya kwa Wote.Katika miongo miwili iliyopita, Rais alisema, hazina hiyo imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 225 nchini Kenya.

“Ushirikiano wetu umekuwa wa ajabu, wamewezesha programu za kimkakati za afya zenye matokeo makubwa nchini,”alibainisha Mheshimiwa Rais Dkt.Ruto.
Mheshimiwa Rais Dkt.Ruto ameyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza katika Ikulu ya Nairobi ambapo alikabidhi zaidi ya mitungi 20,000 ya matibabu ya oksijeni kwa kaunti 47 nchini.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Amref Health Africa, Githinji Gitahi alibainisha kuwa, mitungi hiyo itahudumia angalau vituo 320 vya matibabu nchini.
Rais Dkt.Ruto alisema, dhamira ya Serikali inakwenda zaidi ya utoaji wa huduma za afya za kawaida kwa manufaa ya umma.

"Tunaingilia kati kwa kiasi kikubwa ili kufanya huduma ya afya iwe shirikishi, ipatikane, nafuu na ya ubora wa hali ya juu." Pamoja na uhaba wa rasilimali, Rais alieleza kuwa mpango mpya wa ufadhili umefunguliwa ili kushughulikia changamoto hiyo kwa ufanisi.
Kupitia hafla hiyo, zaidi ya Magavana 20 walikuwepo.Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Anne Waiguru alisema, kaunti zinafuata mikakati ya kuwezesha huduma za afya nchini. "Tunajitolea kutoa huduma bora za afya kwa kila Mkenya kote nchini,"alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news