NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya vituo kwa mabalozi wawili na uteuzi wa balozi mmoja kama ifuatavyo:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amempangia Balozi Humphrey Herson Polepole kuiwakilisha Tanzania nchini Cuba. Kabla ya uteuzi huu Balozi Polepole alikuwa Balozi wa Tanzania, nchini Malawi.
Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Balozi Lt. Jenerali (mstaafu) Yacoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE). Kabla ya uteuzi huu, Balozi Mohamed alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.
Uteuzi na kupangiwa Kituo
Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw. Iddi Seif Bakari kuwa Balozi na kumpangia Ubalozi nchini Uturuki. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Bakari alikuwa Konseli Mkuu nchini Dubai.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 3, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ambapo amebainisha kuwa, tarehe ya uapisho wa Balozi Bakari itatangazwa baadae.