NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Khamis Sued Kagasheki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole kuanzia tarehe 18 Aprili, 2023.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 20, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.
Balozi Kagasheki ni nani?
Mheshimiwa Balozi Khamis Juma Suedi Kagasheki ni miongoni mwa Watanzania waliobobea katika masuala ya diplomasia na siasa ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini tangu 2005. Pia katika Serikali ya Awamu ya Nne aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
Balozi Kagasheki ni mwanadiplomasia ambaye aliwahi kuhudumu katika Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani kati ya mwaka 1977 hadi 1982.
Pia aliongoza Eneo la Uchumi katika Idara ya Sheria na Mashirika ya Kimataifa ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje, Dar es Salaam, Tanzania kuanzia mwaka 1982 hadi 1987.
Baadaye alifanya kazi katika Ubalozi wa Kudumu wa Jamhguri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva nchini Uswisi kati ya mwaka 1987 hadi 1990.
Aidha,Balozi kagasheki alijiunga na Shirika la Haki Miliki Duniani (WIPO) mnamo Januari 1990 na Oktoba mwaka huo huo, akawa Mkurugenzi wa Mahusiano na Mashirika ya Kimataifa na Ukuzaji wa Ubunifu katika Nchi Zinazoendelea.
Mnamo mwaka 1995, alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Rasilimali Watu ya Viwanda na Idara ya Masuala ya Wakala. Mnamo 1997, alikuwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Mipango Mikakati na Maendeleo ya Sera.
Kuhusu Parole
Huu ni utaratibu wa kisheria unaompa fursa mfungwa aliyehukumiwa kutumikia kifungo gerezani cha miaka minne na kuendelea, kutumikia sehemu ya kifungo chake katika jamii kwa masharti maalum baada ya kukidhi vigezo vifuatavyo
i). Awe ametumikia theluthi (1/3) ya kifungo chake na kuonesha mwenendo wa kurekebika kurudi katika jamii kumalizia sehemu ya kifungo chake kwa masharti maalum.
Masharti hayo ni:
- Kuwa chini ya uangalizi maalum kuhakikisha kuwa hatendi kosa lolote mpaka atakapomaliza kifungo chake.
- Kuzingatia masharti ya Parole anayopewa kikamilifu
- Kuwa raia mwema na kuishi kwa kujipatia kipato halali katika jamii.
ii). Awe ameonesha kujutia kosa, kurekebika tabia na kuonesha mwenendo mzuri gerezani.
iii). Mamlaka husika kujiridhisha kuwa hatahatarisha usalama wa jamii.
Sifa
Sheria ya Bodi za Parole Sura 400 ya mwaka 2002 na Kanuni zake za mwaka 1997 inaainisha kuwa mfungwa anayetumikia kifungo cha kuanzia miaka minne (4) na kuendelea anastahili kunufaika na mpango wa Parole kama atakuwa na sifa zifuatazo:-
i. Asiwe amehukumiwa kifungo cha maisha
ii. Asiwe ni mfungwa anayetumikia kifungo kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, madawa ya kulevya na makosa yanayohusiana na kujamiiana.
iii. Asiwe ni mfungwa ambaye kifungo chake kimebatilishwa kutoka kwenye kifungo cha kunyongwa.
iv. Awe anatumikia kifungo kisichopungua miaka minne (4) au zaidi na awe ametumikia 1/3 ya kifungo chake.
v. Awe ameonesha tabia na mwenendo mzuri kwa muda wote aliokaa gerezani.
vi. Asiwe na pingamizi la kimahakama la kukataliwa kunufaika na utaratibu wa Parole chini ya Kifungu cha 67 cha Sheria ya makosa ya Jinai.