Rais Dkt.Samia atoa neno timu ya Wasichana Fountain Gates Dodoma kutwaa ubingwa Afrika

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Wasichana ya Mpira wa Miguu ya Sekondari ya Fountain Gates Dodoma kwa kutwaa ubingwa kwenye Mashindano ya Soka kwa Shule za Sekondari ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF African Schools Continental Champions) upande wa wasichana.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametoa pongezi hizo ikiwa zimepita saa chache baada ya wanafunzi hao kutwaa taji hilo baada ya kushinda mchezo wa fainali dhidi ya Timu ya Wasichana ya Ecole Omar IBN Khatab kutoka Morocco kwa magoli 3-0 huko Durban nchini Afrika Kusini.

"Ushindi wenu unakwenda sambamba na nia ya Serikali kuendelea kuboresha mtaala wa elimu yetu katika kukuza si tu elimu ya darasani, bali pia ya vipaji, ili kupata wahitimu wengi zaidi wenye uwezo wa kutumia maeneo hayo mawili muhimu kuleta maendeleo.

"Nawapongeza Timu ya Wasichana ya Mpira wa Miguu ya Sekondari ya Fountain Gates Dodoma, kwa kutwaa ubingwa kwenye Mashindano ya Soka kwa Shule za Sekondari ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF African Schools Continental Champions), upande wa wasichana,"amefafanua Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.

Aidha, Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Shule za Afrika licha ya taji hilo pia inavuna kitita cha zaidi ya shilingi milioni 690.

Miongoni mwa viongozi walioshuhudiwa mashindano hayo ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe,mawaziri wa michezo kutoka nchi washiriki wa mashindano hayo na Tanzania ikiwakilishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Hamis Mwinjuma na Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news