NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam kwa kuwafunga watani wao Yanga SC mbao 2-0.
Ni kupitia mtanange uliopigwa leo Aprili 16, 2023 katika Dimba la Benjamin Mkapa lillopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
"Hongereni Simba kwa ushindi wenu dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Upinzani wenu wa jadi uwanjani ni burudani inayowaleta pamoja mamilioni ya Watanzania katika kila kona ya nchi yetu, kwa namna ya kipekee;

Mabao ya Simba SC yamefungwa na Henock Inonga dakika ya kwanza na lile la pili Kibu Dennis dakika ya 33. Licha ya Yanga SC kuonesha umahiri ikiwemo kupiga pasi nyingi kulisakama lango la Simba, mambo hayakuwa mazuri kwao.
Aidha, kipindi cha pili Yanga SC walirejea kwa kasi kusaka bao huku Simba wakicheza kwa kujilinda zaidi.
Ushindi huo, unamaanisha Simba SC imefikisha alama 63, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa alama tano na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 26.