Rais Ndayishimiye asisitiza uzalishaji wenye tija kwa kila mtumishi Burundi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Burundi, Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye amewataka wafanyakazi wote wa umma kufanya kazi kwa bidii, hatua ambayo itaongeza uzalishaji ili kufanikisha mchakato wa kuwianishaji mishahara.

Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye ameyasema hayo katika kikao na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi wa sekta ya umma kilichofanyika Jumatano hii katika Ikulu ya Ntare Rushatsi nchini Burundi.

Wakati wa majadiliano yao, washiriki kwa upande wao walichukua nafasi kuwasilisha hali zao kwa kuzingatia ngazi za za wafanyikazi na namna ya kukabliana na hali hiyo kwa kila sekta.

Aidha, Serikali ya Burundi imesema inakusudia kuweka sera ya mishahara ambapo takribani asilimia 94.5 ya wafanyakazi wataongezewa.

Mkuu huyo wa nchi amewataka wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi kuhimiza wafanyakazi kuongeza uzalishaji, suluhu itakayosaidia kutokomeza tofauti za mishahara nchini.

Pia aliwataka kufanya kazi kwa kujikita katika mwelekeo wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Burundi ya 2040 na mwelekeo wa 2060, ili matokeo bora yaweze kupatikana kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Napendekeza muwapange watumishi wa umma ili kila mmoja awe na mpango kazi wa kufuata,”alisisitiza Mheshimiwa Rais Ndayishimiye akiwataka kusimamia suala la mishahara kwa uwazi na kuwaambia kuwa wajibu wao wa chama si kukuza harakati za mgomo badala yake kuongeza uzalishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news