Rais Ramaphosa afanya uteuzi Shirika la Utangazaji la SABC

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Afrika Kusini,Cyril Ramaphosa kwa mujibu wa kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Utangazaji ya mwaka 1999 (Sheria Na.4 ya 1999) kama ilivyorekebishwa amefanya uteuzi wa wajumbe wasio watendaji wa Bodi ya Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) kwa miaka mitano.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 18, 2023 na Msemaji wa Rais, Ramaphosa, Bw.Vincent Magwenya ambapo amefafanua wajumbe hao wanaanza majukumu yao kuanzia tarehe ya kuchapishwa kwa notisi katika Gazeti la Serikali.

Walioteuliwa na Mheshimiwa Rais Ramaphosa ni Dkt.Renee Horne,Adv Tseliso Thipanyane,Bw.Khathutshelo Ramukumba,Bi.Nomvuyiso Batyi;Bi.Phathiswa Magopeni,Mheshimiwa Aifheli Makhwanya,Bi.Magdalene Moonsamy.

Pia yupo,Bi.Rearabetsoe Motaung, Mheshimiwa David Maimela,Bw.Dinkwanyane Mohuba,Bw.Mpho Tsedu na Bi.Palesa Kadi.

Kwa mujibu wa kifungu cha 13(3) cha Sheria hiyo, Rais Ramaphosa amemteua Bw.Khathutshelo Ramukumba kuwa Mwenyekiti na Bi.Nomvuyiso Batyi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya SABC.

“SABC ni taasisi muhimu ya demokrasia yetu ya kikatiba. Ninaamini wajumbe wapya wa bodi watafanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha kuwa Afŕika Kusini inaendelea kunufaika kutokana na chombo hicho cha utangazaji cha umma thabiti, huru na chenye ufanisi,”amesema Rais Ramaphosa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news