NA DIRAMAKINI
RAIS wa Baraza la Mitume na Manabii Tanzania,Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliongoza Taifa kwa mafanikio makubwa licha ya changamoto mbalimbali zinazoendelea kuikabili Dunia kupitia nyanja tofauti tofauti ikiwemo za kijamii na kiuchumi.
Dkt.Nabiijoshua ametoa pongezi hizo Aprili Mosi, mwaka huu katika Kongamano la Kitaifa la Mashangilio ya Baraza la Mitume na Manabii Tanzania ambalo limefanyika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
"Nitakua sijatenda mema kama sitamshukuru kipekee sana mama yetu, Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Serikali yake anayoiongoza.
"Kwani,pamoja na changamoto nyingi ambazo taifa letu linapitia juu ya mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa,kwa mafanikio makubwa bado hekima, umoja na amani zimebakia kuwa ndiyo ngao kuu za ulinzi wa usalama na ustawi wa taifa letu.
"Bila kusahau undungu, mshikamano,mila na desturi zetu zinazoishangaza Dunia wakati wote.Asante sana Mhe.Rais na mama yetu, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wa kuzienzi tunu hizi za utu na ubinadamu wetu walizotuachia waasisi wa Taifa letu hili jema la Tanzania,

"Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Abeid Amani Karume, ambayo wewe ndiye kiongozi wake mkuu wa kwanza mwanamke na mwenye moyo halisi wa mama Tanzania, Mungu akubariki sana mama yetu mwema sana,"amefafanua Rais Dkt.Nabiijoshua.
Katika hatua nyingine, Rais Dkt.Nabiijoshua amemshukuru Mungu kwa kuendelea kuwaunganisha mitume na manabii Tanzania kwa ajili ya kuujenga Mwili wa Kristo, kuhubiri na kueneza habari njema ya neno la Mungu mijini na vijijini.
"Mungu, amedhihirisha furaha yake kwetu kwa kutufanya wamoja kama tulivyo hivi leo.Nawashukuru wazee wetu kwa kuunga mkono jitihada hizi za Umoja wa Mitume na Manabii Tanzania, asanteni sana kwa upendo wenu huo.
"Mitume na manabii natambua kuwa tumefika hapa leo kwa sababu wote tumelipa gharama za umoja wetu huu. katika kulipa gharama hizo, wengi mmeumizwa sana kila mtu kwa namna yake nawasihi sameheni yote kwa maana sasa yamekuwa mapya.
"Ndugu zangu mitume na manabii, mashangilio haya hatutashangilia bure. Katika mfuko wangu wa kichungaji nimebeba nakala ya cheti cha usajili wa baraza ambalo ni chombo halali cha mitume na manabii wote Tanzania pamoja na makundi mengine madogo ya imani za kilokole walio nje ya TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania), CCT (Baraza la Jumuiya ya Kikristo Tanzania) na CPCT (Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania).
"Tumefikia hapa tulipo kwa sababu Mungu asiyedhihakiwa alimwandaa mzee wetu mtume na mpiganaji mkuu wa vita vya nyikani Profesa Paul Zemu Shemsanga, mlezi wetu mkuu na mtu shujaa asiyerudi nyuma kabla ya ushindi kupatikana Baba yetu Askofu Dkt.Dastan Haule Maboya, mzee wetu mlezi wa mkoa wa Kilimanjaro, Bishop Mwanga na wazee wengine waliokuwa mstari wa mbele katika kutusaidia kufanikisha chombo hiki kinacholetwa kwenu kwa utukufu wa Mungu wetu wa milele na milele.
"Kwa maumivu makubwa waliijenga safina ambayo sisi kuanzia leo tutakaa ndani yake wakati gharika ikiendelea huko nje,"amefafanua Rais Dkt.Nabiijoshua.
Wakati huo huo, Rais wa Baraza la Mitume na Manabii Tanzania, Dkt.Nabiijoshua ametoa wito kwa mitume na manabii kusimama imara kupiga vita hamasa ya mapenzi ya jinsia moja, vitendo ambavyo siku za karibuni vimeshika kasi duniani.
"Dunia yetu hivi sasa imekumbwa na wimbi la usodoma na gomora, watu wanausambaza ushoga na usagaji kwa gharama ya kununua Dunia yote iwe mali yao ya kishetani, pamoja na watu wote waishio humo. Hii ni dhambi kubwa mbele za Mungu kwa kawaida dhambi huwa haitosheki hadi izae mauti.
"Tusipochukua hatua za haraka na ukali unaohitajika kuiondoa hii dhambi katika nchi yetu, amin...amin nawaambia siku si nyingi vijana wetu watalazimishwa kuoana na wanyama na hawa ni wengine wa mwituni wa mapori ya dunia hii.
"Ndugu zangu mitume na manabii ili kushinda vita hii hatuna budi kumlilia Mungu, kufundisha, kuonya, kumea na kukaripia dhambi hii kwa nguvu zote.
"Natoa wito huu mkubwa kwenu, tukiiachia Serikali peke yake jambo hili ni zito litailemea kabisa. Ni wajibu wetu sote kusema basi na kuungana na madhehebu mengine ya dini nje ya imani zao kwa ajili ya taifa letu, wakiwemo waislamu ambao kwenye jambo hili haramu linalokosoa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, wameonyesha kwa vitendo kwamba watalipa gharama za kulipinga kwa uwezo wao wote kabisa,"amefafanua Rais Dkt.Nabiijoshua.
Ameendelea kufafanua kuwa, "Sasa naomba niwarudishie furaha yenu kwamba, baraza hili linalounganisha mitume na manabii wote Tanzania hadi sasa linamiliki vyuo vikuu viwili vya theolojia.
"Japan Bible Institute-Graduate School of Theology ambayo imeruhusiwa kuendesha mafunzo yake ya kidini na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Tume ya Vyuo Vikuu vya Kikristo Ulimwenguni.
"Chuo kinatoa certificate hadi PHD za elimu ya Kikristo. Jumla ya kozi ni 55, pia baraza limesimamia lugha mpya ya Kiungu ya TACHIL.
"Hivyo, naomba wenyeviti wote wa mikoa na wilaya zote muwe tayari kusimamia majukumu ya kiuongozi na kuwezesha mitume na manabii wote ili kuhakikisha wanajiunga na vyuo vyetu hivyo ili kujiongezea elimu, maarifa na ujuzi zaidi katika huduma zetu.
"Na sasa tuna uwezo wa kuwadhamini watumishi wa Mungu wenye huduma ambazo hazijasajiliwa, nitawalea hadi watakapopata usajili serikalini.
"Pia naomba niwashukuru vyombo vya habari na wamiliki wao ikiwemo TOPTV+ kwa kujitolea kwenu kurusha matangazo haya ili umma wa watanzania uweze kupata taarifa sahihi kuhusu mwili wa Kristo Tanzania. Asanteni sana,"amesisitiza Rais Dkt.Nabiijoshua.