
Mwezi wa Ramadhani ni wakati wa uchamungu ambapo Waislamu hufunga, kuswali, kusoma Quran tukufu, na kufanya Tarawehe.
Baada ya kuhitimika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, leo Aprili 22, 2023 ni Sikukuu ya Eid-ul-Fitr ambapo uongozi wa DIRAMAKINI unawatakia Waislamu na Watanzania wote sikukuu njema, kubwa zaidi tuendelee kudumisha amani, upendo na mshikamano kwa ustawi bora wa Taifa letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.