NA DIRAMAKINI
BAADA ya utumishi wake wa miaka 20 ndani ya Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), mtangazaji mbobezi ndugu Salim Kikete ametangaza kustaafu kazi katika shirika hilo.
Ndugu Kikeke ambaye ni Mtanzania ameaga rasmi Aprili 28, 2023 wakati akitamatisha kipindi maarufu zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki cha Dira ya Dunia na kusema kuwa, anakwenda kufanya majukumu mengine ingawa hajayaweka wazi.
"Nimekuwa na wakati mzuri hapa London tangu nilipojiunga na BBC nikiwa redio, kisha televisheni, ninakwenda kufanya majukumu mengine na leo hii ndio itakuwa mara yangu ya mwisho leo kutangaza Dira ya Dunia. Ninawashukuru wafanyakazi niliokuwa nikifanya nao kazi hapa BBC na vyombo vingine vya habari nilivyofanya nao kazi kabla sijaja hapa, wote mmenisaidia sana kutimiza ndoto zangu na kunifikisha hapa nilipo leo,"amefafanua Kikeke.
Ndugu Kikeke ni kati ya vijana wa Kitanzania ambao wanaonekana kupambana hadi kuweza kujenga majina na heshima zao duniani bila kukata tamaa.
Hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari likiwemo gazeti la Mwananchi likieleza kuwa, Kikeke baada ya kumaliza Stashahada ya Umwagiliaji katika Chuo cha Kilimo Nyegezi, Mwanza alikutana na changamoto kadhaa hasa ya kukosa ajira kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu mfululizo.
”Nilimaliza Stashahada yangu mwaka 1994 kozi ya Umwagiliaji, kwa sasa labda ningekuwa bwana shamba au mfanyakazi wa kilimo,” anasema Kikeke.
Baada ya kumaliza chuo, juhudi za kusaka ajira zilikuwa ngumu.Kwa karibu mwaka mzima wa 1995, alikwenda katika machimbo ya Tanzanite ya Mererani Arusha. “Hakukuwa na ajira na kishawishi cha kujiingiza katika uhalifu kilikuwa kikubwa,” anasema bila kueleza zaidi.
Katika hatua ya kuepuka mazingira hayo aliamua kuwa ‘Mwanaapolo’ kama wanavyojulikana wachimbaji wa Tanzanite yaani kutumika kuingia kwenye mashimo kubeba mizigo au kazi nyingine migodini. Baada ya kushauriwa na mama yake kuondoka mchimboni, alirejea Dar es Salaam.
Aidha, katika kipindi hicho Kikeke anasema alikuwa akishinda kijiweni mitaa ya Sinza Kumekucha akiwa na rafiki yake, Joseph Mboya ambaye kwa sasa ni marehemu.
“Mboya ndiye mmoja kati ya rafiki zangu ambao tulibadilishana mawazo, tulifarijiana na kufikiria matarajio ya ndoto zetu, mambo yalikuwa magumu mpaka nikafikia hatua ya kusema basi imetosha,” anasema Kikeke.
Kuingia utangazaji
Mara baada ya kuona matumaini yakififia kupitia taaluma yake ya kilimo, Kikeke aliamua kubadilisha ukurasa wa maisha baada ya kupiga hodi katika ofisi za kituo cha TV cha CTN ambacho kilikuwa na redio wakati huo ikijulikana kama Classic FM ambayo kwa sasa ni Magic FM.
Sababu, nia na ujasiri wa kuchukua uamuzi huo, haikutokea kama ajali, bali ilitokana na ushawishi aliokuwa ameupata kutoka kwa mama yake mzazi ambaye ni marehemu kwa sasa.
“Mama yangu alikuwa wa kwanza kunijengea uwezo wa kuingia katika utangazaji, alikuwa anapenda sana kusikiliza habari za redioni na alinishawishi kufuatilia kila habari iliyokuwa inaendelea duniani, nikawa na uwezo wa kutamka maneno vizuri na kusoma habari,” anasema Kikeke.
Ilikuwa ni mwishoni mwa 1997, Kikeke alifika katika ofisi za kituo cha kurusha matangazo cha CTN. “Kwa sasa wanaita Magic FM, walikuwa wanafungua kituo kipya cha Classic FM hivyo niliomba kufanya kazi bure, nikapewa kipindi cha kucheza miziki ya Kiingereza,” anasema Kikeke.
Anasema, baada ya kupata uhakika wa kuendelea na kazi hiyo, Januari mwaka 1998 aliamua kwenda kusoma kozi fupi ya utangazaji habari katika chuo cha uandishi wa habari cha Tanzania School of Journalism (TSJ).
”Pale nilisoma cheti kwa miezi mitatu na kurudi tena kazini, nikaanza kusoma habari za Kiingereza na Kiswahili wakati mwingine nilikuwa naenda kutafuta habari. Hata hivyo mwezi mmoja baadaye wakanifukuza kazi kwa sababu ambazo nisingependa kufafanua zaidi,” anasema.
Kikeke baada ya kufukuzwa kazi, hakuishia kulia mtaani, badala yake alianzisha mkakati wa kusaka ajira tena kwenye taasisi yenye hadhi ya juu zaidi, Radio Tanzania (RTD) ambayo sasa ni Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), hiyo ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka 1998.
”Kwa kipindi hicho Abdul Ngarawa alikuwa mkurugenzi wa RTD, nikapelekwa idhaa ya Kiingereza, ‘English Service’, na kuandaa vipindi vya muziki kila siku kuanzia saa 12:00 jioni mpaka saa 6:00 usiku,” anasema Kikeke na kufafanua kuwa alikuwa akifanya kazi kwa muda ‘part-time.
Alianza kupangiwa vipindi vya kutangaza baada ya kukaa kwa zaidi ya mwaka mmoja. “Baadaye nikapewa kipindi cha Mwelekeo kilichoanzishwa wakati wa maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, nilikuwa mtangazaji wa mwanzoni kabisa katika kipindi hicho,” anasema Kikeke.
Katika kipindi hicho, Radio Tanzania walianzisha kituo cha matangazo cha FM, kiitwacho PRT kikitoa matangazo kwa lugha ya Kiingereza.
RTD na Kituo cha PRT ndizo kwa sasa zinafahamika kama TBC na TBC1. “Mimi nikaondoka pale na kurudi tena CTN,” anasema.
Baada ya kurudi katika kituo hicho, Kikeke alifanikiwa kupata nafasi ya kusoma habari kwenye TV mpaka mwezi Agosti wakati kampuni hiyo ilipouzwa na kuwa chini ya kituo cha Channel Ten na DTV. Baadae alihamia ITV.
Aidha, baada ya hapo alifanikiwa kuandika barua ya maombi ya kazi katika Kituo cha Radio One. “Kwa wakati huo Charles Hilary ndiye alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Radio One, akaniomba nimpatie mfano (Demo) ya kipindi chochote nilichowahi kufanya, kwa bahati mbaya sikuwa na ya radio ila nikawa na ya TV,”anasema Kikeke.
Anaongeza kuwa, hali hiyo ikamfanya abadilishe mlango wa kutoka Redio One na kuingia ITV. “Charles Hilary akaipeleka ile demo upande wa televisheni ya ITV, kulikuwa na Betty Mkwasa na Joyce Mhaville, wakaipenda kazi yangu na kuagiza niripoti pale kazini,”anasema.
Kikeke alipangiwa jukumu la utangazaji wa vipindi vya taarifa za habari kila siku na habari za ‘Jiji Letu’ hata hivyo mambo yalibadilika kwa muda mfupi pale ofisini.
Safari ya BBC
Radio One walikuwa ni Redio washirika wa BBC hivyo walikuwa na mkataba wa kuchukua mtangazaji mmoja kila mwaka na kumpeleka kufanya kazi makao makuu ya BBC kwa muda wa miezi kadhaa. "Mwezi Mei 2003 nikafaulu majaribio ya kuingia BBC," ambako amehitimisha majukumu yake tayari baada ya kuaga wafuasi wake Aprili 28, 2023. (Mashirika/Mwananchi)