NA MWANDISHI WETU
SERIKALI kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 inaendelea na mchakato wa kuboresha hifadhi changa 17 za Taifa ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara, huduma za malazi na chakula na maeneo ya uwekezaji kwa lengo la kukuza utalii na kuongeza mapato.

Amezitaja Hifadhi za Taifa zinazoboreshwa kuwa ni Burigi-Chato, Gombe, Ibanda-Kyerwa, Katavi, Kigosi, Kisiwa cha Rubondo, Kisiwa cha Saanane, Kitulo, Milima ya Mahale, Milima ya Udzungwa, Mikumi, Mkomazi, Mto Ugalla, Nyerere, Ruaha, Rumanyika-Karagwe na Saadani.
Aidha, amefafanua kuwa maboresho yanayofanywa katika hifadhi hizo yanaenda sambamba na utekelezaji wa Programu ya Tanzania – the Royal Tour ambapo kwa sasa Serikali imejikita zaidi kwenye maeneo mapya ya utalii.