NA DIRAMAKINI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Angellah Kairuki amesema, Serikali imendaa Sera ya Ugatuaji wa Madaraka (D by D) ambayo iko katika hatua ya mwisho ya mapitio inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Mheshimiwa Kairuki ameyasema hayo Aprili 4, 2023 jijini Dodoma wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika Mkutano Mkuu wa 13 wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA).
Amesema, kukamilika kwa sera hiyo kutasaidia kupunguza au kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili TOA hasa kuwapa nguvu Mamlaka za Serikali za Mitaa kukusanya mapato kupitia ushuru, ada na tozo mbalimbali (levy taxes, fees and charges) badala ya kutegemea fedha kutoka Serikali kuu.
"Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuhusu Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG), ulikuwa ni mfumo muhimu kwa ajili ya kupeleka fedha za maendeleo kwenye Mamlaka za Serikali Mitaa (MSM) Tanzania Bara, kama nyenzo ya utekelezaji wa ugatuaji wa madaraka sehemu ya fedha,"amefafanua Waziri Kairuki.
Pia amesema,tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004/2005, mfumo huo ulichangia kwa kiasi kikubwa kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Aidha,ulileta msukumo kwenye maeneo ya utendaji wa Majukumu ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo mipango, bajeti, usimamizi wa fedha pamoja na sekta nyingine kama Afya, Elimu, Maji na Kilimo.
"Mfumo wa LGDG ulikuwa mfano wa kuigwa kwa ufadhili wa uwekezaji wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, kulikuwa na ongezeko la upatikanaji wa rasilimali fedha za maendeleo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na ndiyo ruzuku iliyowezesha kukamilisha maboma yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.
"Ndiyo ruzuku iliyotumika kuendesha ofisi na kujenga uwezo wa watendaji katika ngazi za kata,vijiji na mitaa na ndiyo fedha zilizotumika katika ufuatiliaji wa miradi kwa uhakika na kutekeleza miradi iliyoibuliwa na jamii,"amebainisha Waziri Kairuki.
Mheshimiwa Waziri Kairuki amesema, Mfumo wa LGDG ulihuishwa mwaka 2015/2016 na ulipaswa kuanza mwaka 2016/2017.
Hata hivyo, amesema Serikali ilikuja na mpango wa miradi ya kimkakati kwa lengo la kuzalisha mapato katika Halmashauri ili ziweze kujiendesha na kusitishwa kwa mfumo wa Ruzuku ya Maendeleo katika Serikali za Mitaa.
"Mheshimiwa Waziri Mkuu, pamoja na uwepo wa miradi ya kimkakati, ruzuku ya fedha za LGDG bado ni muhimu kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwani fedha hizi zitasaidia kukamilisha miradi ya maendeleo ambayo wananchi wanaendelea kutekeleza.
"Fedha za LGDG hutumika kuunga mkono jitihada na kupunguza miradi ambayo haikukamilika, kuimarisha mfumo wa upimaji unaozingatia utendaji wa kazi na matokeo zaidi pamoja na mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) na kuwajengea wananchi na watendaji uwezo na kubadili mtazamo wa utegemezi kwa Serikali,"amefafanua.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Waziri Kairuki amesema,kwa kutambua umuhimu huo, OR-TAMISEMI inaendela kuangalia namna bora ya kutekeleza LGDG iliyoboreshwa.
Vile vile amefafanua kuwa, OR - TAMISEMI pamoja na watalam kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) wameandaa miongozo mbalimbali inayoelekeza namna bora ya kushirikisha wananchi katika shughuli zote za maendeleo hapa nchini.
"Bado OR -TAMISEMI inasisitiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kutumia vizuri miongozo hiyo ili kusaidia uhamasishaji wa kina kwa Wananchi utakaozaa umiliki na uendelevu wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika maeneo yao.
"Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba tena nitumie nafasi hii kuwaomba Makatibu Tawala wa Mikoa yote, Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wote nchini kutumia Mfumo wa Fursa na Vikwazo ulioboreshwa (improved O&OD) ili kuongeza uwazi na uwajibikaji hususani katika Vitongoji, Vijiji na Mitaa,"amebainisha Mheshimiwa Waziri Kairuki.
Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki alitambua mchango mkubwa wa Serikali ya Japan kwa kuwawezesha takribani watumishi 6,367 kupata mafunzo ya kubadilishana uzoefu wa namna bora ya ugatuaji wa madaraka kwenye ngazi ya msingi.
Amesema, Serikali ya Japan imeendelea kufadhili progamu hiyo tangu 2006 hadi sasa. "Tunawahakikishia kuwa uzoefu tuliopata kutoka kwao tutautumia katika kuboresha uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa hapa kwetu Tanzania,"amesema Waziri Kairuki.